Pata taarifa kuu
ISRAEL

Shambulizi la kigaidi nchini Bulgaria laua raia 7 wa Israel

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameishutumu Iran kupanga na kutekeleza shambulizi la kigaidi dhidi ya raia wake waliokuwa nchini Bulgaria kwenye shughuli za kiutalii.  

Matangazo ya kibiashara

Raia saba  wa Isreal waliuawa katika shambulizi hilo na kuwajeruhi wengine 30,huku walioshudia shambuzli hilo wakieleza namna walivyowaona  abiria wakikimbia na kuruka nje kupitia madirisha ya basi walilokuwa wanasafiria.

Serikali ya Bulgaria imetangaza kuanza uchunguzi wa kina kubaini ni nani waliotekeleza shambulizi hilo ambalo limetajwa kubeba sura ya kigaidi na kusababisha makundi kadhaa kujumuishwa.

Waziri wa Ulinzi wa Israel Ehud Barak amesema hakuna ubishi wa aina yoyote kwamba shambulizi hilo ni la kigaidi na nchi ya Iran au Makundi ya Waislam yenye msimamo mkali yamehusika,kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma nchini Kenya,India,Thailand, Azerbaijan, na  Cyprus kulenga raia wa Israel.

Rais wa Marekani naye  Barrack Obama ameshtumu shambulizi hilo na kueleza kuwa Marekani itaendelea kushirikiana na Israel kupambana na ugaidi duniani.

Hili ndilo shambulizi baya zaidi kuwahi kuwakumba raia wa Isreal nje ya taifa lao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.