Pata taarifa kuu
SYRIA

Waziri wa Ulinzi wa Syria auliwa

Waziri wa Ulinzi wa  Syria Jenerali Daoud Rajha, ameuliwa baada ya kutokea kwa shambulizi la bomu la kujitoa mhanga katika ofisi za usalama wa ndani mjini Damascus.

Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hilo pia limesabisha kuuawa kwa shemeji wa rais Bashar Al Assad Assef Shawkat ambaye pia ni afisaa wa juu wa jeshi nchini Syria.

Shambulizi hilo lilitokea wakati Waziri huyo wa alipokuwa anahudhuria kikao na viongozi wengine wa kijeshi na Waziri wa Mambo ya ndani Mohammed al-Shaar aliyejeruhiwa .

Tayari rais Bashar Al Assad amemteua Fahd al-Freij kuwa Waziri mpya wa Ulinzi,huku maafisa wa usalama wakisema kuwa aliyetekeleza shambulizi hilo huenda ni mlinzi wa karibu wa rais Assad.

Shambulii hilo linatokea huku wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN jumatano hii linatarajiwa kupiga kura kupitisha azimio lenye lengo la kumaliza machafuko na umwagaji wa damu ambao unaendelea kushuhudiwa nchini Syria.

Baraza la Usalama linapiga kura hiyo ikiwa zimesalia siku mbili kabla ya kwisha kwa muda ambao ulikuwa umewekwa na Mpatanishi wa Mgogoro wa Syria Kofi Annan wa kutaka kutekelezwa mapendekezo yake sita ya kumaliza machafuko

Muda huo itamalizika siku Ijumaa ya juma hili huku hakuna chochote ambacho kimeshatekelezwa na badala yake mauaji ya kinyama pamoja na mapigano vikiendelea kutekelezwa nchini Syria kwenye Miji mbalimbali.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.