Pata taarifa kuu
SYRIA

Baraza la usalama la UN latakiwa kushughulikia mauaji Syria.

Mjumbe wa amani nchini Syria kutoka Umoja wa mataifa Koffi Annan amesema Syria imekiuka maazimio ya baraza la usalama la umoja wa mataifa baada ya mauaji ya halaiki huko Tremsa wakati huu ambapo katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon akilitaka jeshi la UN kukomesha umwagaji damu nchini humo.

Baadhi ya miili ya raia waliouawa kijijini Tremsa nchini Syria
Baadhi ya miili ya raia waliouawa kijijini Tremsa nchini Syria AFP/YOU TUBE
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa wanaharakati wa haki za binadamu takribani watu 150 wameuawa katika mauaji ambayo yanadaiwa kujiri baada ya mapambano baina ya majeshi ya serikali dhidi ya waasi.

Naye katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki moon amelitaka baraza la usalama la umoja wa mataifa kushughulikia machafuko hayo yaliyodumu kwa zaidi ya miezi 16 sasa na kuonya kuwa kushindwa kutekeleza ni kuruhusu mauaji zaidi kutokea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.