Pata taarifa kuu
PAKISTAN-AFGHANISTAN-MAREKANI

Msafara wa Malori ya kwanza ya Majeshi ya NATO wavuka mpaka wa Pakistan kuelekea Afghanistan

Malori ya kwanza yaliyosheheni maji safi na salama mali ya Majeshi ya Kujihami ya nchi za Magharibi NATO yamevuka mpaka kutoka Pakistan na kuingia nchini Afghanistan ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miezi saba iliyopita.

Malori ya Majeshi ya NATO yakivuka mpaka wa Pakistan na kuingia nchini Afghanistan kwa mara ya kwanza
Malori ya Majeshi ya NATO yakivuka mpaka wa Pakistan na kuingia nchini Afghanistan kwa mara ya kwanza
Matangazo ya kibiashara

Malori ya matatu ndiyo yamekuwa ya kwanza kuvuka mpaka wa Pakistan kueleka Afghanistan njia ambayo itakuwa inatumika kwa ajili ya kusafirisha zana mbalimbali za NATO kuendelea operesheni yao huko Kabul.

Malori zaidi yanatarajiwa kuvuka mpaka kuelekea nchini Afghanistan yakipitia Pakistan baada ya kufikiwa makubaliano baina ya serikali ya Marekani na ile ya Islamabad ya kufunguliwa kwa mipaka yake.

Hatua ya kufunguliwa kwa mpaka wa Pakistan kuruhusu malori ya NATO kuelekea nchini Afghanistan inatajwa itasaidia sehemu kubwa ya mpango wa kuendeleza operesheni za kijeshi zenye lengo la kurejesha utulivu.

Malori zaidi yameendelea kuwepo katika Bandari ya Karachi iliyopo nchini Pakistan yakisubiri taratibu zikamilike kabla ya kuanza safari ya kuvuka mpaka wa nchi hiyo kuelekea Afghanistan.

Pakistan imefikia hatua ya kufungua mpaka wake kuruhusu malori ya Majeshi ya NATO kuelekea Afghanistan baada ya Marekani kuomba radhi kutokana na kuhusika kuwaua wananchi ishirini na wanne mwezi Novemba.

Vifo hivyo vilichochea kutetereka kwa uhusiano wa kidiplomasia baina ya Marekani na Pakistan lakini sasa Islamabad inasema kuna uwezekano uhusiano baina yao na Washington utaimarika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.