Pata taarifa kuu
SYRIA-UTURUKI

Katibu wa NATO Andres Fogh Rasmussen ataka suluhu ya mgogoro wa kisiasa nchini Syria ipatikane

Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi NATO imeishauri nchi ya Syria kutafuta suluhnu ya mgogoro wake wa kisiasa na kuionya juu ya tukio la kushambulia ndege ya kivita ya Uturuki ambayo ilikatiza kwenye anga lao.

Katibu Mkuu wa NATO Andres Fogh Rasmussen ambaye ametaka suluhu ya kisiasa ipatikane nchini Syria
Katibu Mkuu wa NATO Andres Fogh Rasmussen ambaye ametaka suluhu ya kisiasa ipatikane nchini Syria
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen amesema ana imani Mamlaka nchini Syria zitafanya kila linalowezekana katika kuhakikisha inamaliza hali inayoendelea kwa sasa na kuchangia kutokea kwa machafuko.

Fogh Rasmussen ameongeza kuwa ni lazima nchi ya Syria ijiepusha na tatizo hilo la kisiasa sambamba na kujizuia kuingia kwenye mgogoro na jirani zao wa Uturuki ambao wamechukizwa na kutunguliwa kwa ndege yao.

Katibu Mkuu wa NATO amebainisha kuwa kitendo cha kutunguliwa kwa ndege ya kivita ya Uturuki hakukubaliki na wanaangalia ni kwa namna gani ndege hiyo imetunguliwa kabla ya kuchukua hatua zaidi.

Fogh Rasmussen akizungumza na Waziri Mkuu wa Slovenia Janez Jansa amesema NATO wanajiandaa kuhakikisha wanamlinda mwanachama wao Uturuki iwapo watahitajika kufanya hivyo kwa usalama wa nchi hiyo.

Mkuu huyo wa NATO amesema tangu awali wameshakubaliana hawawezi wakatumia jeshi katika kupata suluhu ya mgogoro wa Syria na badala yake wanataka uwepo wa suluhu ya kisiasa na si kinyume cha hapo.

Fogh Rasmussen naye hakuwa mbali na mpango ambao umekuwa ukipendekezwa na baadhi ya nchi na Mpatanishi wa Mgogoro wa Syria Kofi Annan ambao wote wanataka Rais Bashar Al Assad akae kando na serikali ya umoja wa kitaifa iundwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.