Pata taarifa kuu
PALESTINA

Rais wa Palestina Abbas atangaza kufanyika kwa uchunguzi dhidi ya kifo cha Hayati Yasser Arafat

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amesema serikali yake ipo tayari kuruhusu kufukuliwa kwa mwili wa Hayati Yasser Arafat ufukuliwe baada ya uwepo wa madai ya sumu kutumika kumuua Kiongozi huyo wa zamani. Msemaji wa Rais Abbas, Nabil Abu Rudeinah amesema Mamlaka nchini Palestina zitawatumia watalam wa Masuala ya Kisayansi kutoka nchi za Kiarabu na wale wa Kimataifa kupitia ushahidi uliowasilishwa.

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ametangaza kufanyika uchunguzi juu ya kifo cha Hayati Yasser Arafat
Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ametangaza kufanyika uchunguzi juu ya kifo cha Hayati Yasser Arafat
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi uliofanywa kwa kipindi cha miezi tisa na Kituo kimoja Cha Habari umegundua kifo cha Arafat aliuawa kwa kutumia sumu aina ya polonium ambayo iliweka kwenye nguo zake na mswaki.

Msemaji wa Rais Abbas amesema uwepo wa uzumi wa kuuawa kwa Arafat kwa kutumia sumu ni lazima ufanyiwe kazi ili kubaini kama kuna ukweli wowote wa madai ambayo yamezuka na kuleta utata.

Uchunguzi huo wa awali ambao umezua hofu nchini Palestina na inasemekana kuna mionzi maalum ambayo ilitumiwa katika kufanikisha kifo hicho kwa kutumia madini maarufu sana ya polonium.

Katika hatua nyingine uchunguzi huo wa mwili wa hayati Arafat utafanyika ikiwa tu wanafamilia nao wataridhia kufukuliwa kwa mwili wa mpendwa wao ili kubaini kama kweli sumu ilitumika kutekeleza kifo chake.

Kiongozi anayeongoza Jopo la Uchunguzi huo Tawfiq Tirawi ametoa kauli hiyo baada ya kuongezeka kwa shinikizo likitaka kubaini kile ambacho kimechangia kifo cha Hayati Arafat.

Tirawi amesema licha ya Rais Abbas kuridhia kufanyika kwa uchunguzi huo lakini hana mamlaka ya kuishinikiza familia kukubaliana na hilo kwa hiyo ni lazima ipatikane ridhaa ya wanandugu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.