Pata taarifa kuu
ULAYA

Viongozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya zajipanga kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi

Viongozi wa nchi za Jumuiya ya Ulaya, EU wameanza mkutano wao wa siku mbili mjini Brussells ukiwa na lengo la kuangalia njia za kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi na madeni unaozikabili nchi hizo.Akifungua mkutano huo rais wa EU, Herman Van Rompuy amesema kuwa wananchi wa jumuiya hiyo wana matarajio makubwa kutoka kwa viongozi hao kuwa watafanikiwa kukabiliana na matatizo mbalimbali yanayozikabili nchi hizo za Ulaya.

REUTERS/Michel Euler/Pool
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wa nchi 27 za EU wameanza mkutano wao huo huku dunia ikisubiri kwa hamu kufahamu mpango kabambe wa kunusuru sarafu ya Euro isiendelee kuporomoka.

Katika mkutano huo Waziri mkuu wa Ubeligiji Elio Di Rupo ameungana na viongozi wenzake wa Ulaya kusema kuwa nchi za EU hazina chaguo bali kuwa na mpango wa dharura utakaosaidia nchi hizo kuondokana na matatizo ya kiuchumi.

Katika mkutano huo viongozi wa Ufaransa na Ujerumani wamesitiza umoja na ushirikiano kama nchi za EU zinataka kumaliza matatizo yake huku rais wa ufaransa Francois Hollande akisema kuwa lazima zichukuiwe hatua madhubuti na za haraka ili kukabiliana na matatizo hayo.

Kansela wa ujerumani Angela Merkel kwa upande wake anaona kuna umuhimu wa kubana matumizi na kuwa na mipango ya muda mrefu ya kufufua uchumi ambao umedorora ikiwa ni pamoja na kuimarisha umoja wa sarafu ya EURO unaoelekea kuyumba.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.