Pata taarifa kuu
KENYA

Idadi ya vifo vilivyotokana na shambulizi la guruneti nchini Kenya yaongezeka.

Idadi ya vifo vilivyotokana na shambulizi la guruneti katika baa moja mjini Mombasa nchini Kenya imeongezeka na kufikia watu watatu leo Jumatatu na majeruhi thelathini bado wanapatiwa matibabu hospitalini, ikiwa ni pigo jipya katika juhudi za serikali katika kuimarisha usalama wa taifa na kufufua utalii. 

Mmoja wa majeruhi katika shambulio la guruneti katika baa ya Jericho.
Mmoja wa majeruhi katika shambulio la guruneti katika baa ya Jericho. news.terra.com
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya Nelly Muluka amesema kuwa watu wawili wamefariki wakiwa Hospitalini na mmoja amefariki mapema katika eneo la tukio.

Hapo awali polisi walisema kuwa mtu mmoja amefariki katika mlipuko uliotokea kwenye bar ya Jericho wilayani Mishomoroni, wakati mashabiki wa soka walipokuwa wakitazama robo fainali ya mashindano ya Euro 2012 kati ya Uingereza na Italia.

Hivi karibuni katika mfululizo wa mashambulizi hayo katika taifa hilo la Afrika Mashariki, kundi la waasi wa kiislam kutoka Somalia la Boko Haramu linadaiwa huenda limehusika na shambulio hilo ambalo limetokea baada ya kutolewa kwa tahadhari maalum kwa wageni ambao walitaka kusafiri nchini Kenya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.