Pata taarifa kuu
SYRIA

Syria yakiri kuitungua ndege ya kivita ya Uturuki.

Syria imethibitisha kuiangusha ndege ya kivita ya Uturuki iliyoingia katika mipaka yake na hivyo kuzua mgogoro mpya kati ya nchi hizo mbili huku ikiwashutumu waasi kwa kuwaua wafuasi 25 wa serikali.

File photo of Turkey's Prime Minister Recep Tayyip Erdogan addressing the audience during the presentation in Ankara March 1, 2012.
File photo of Turkey's Prime Minister Recep Tayyip Erdogan addressing the audience during the presentation in Ankara March 1, 2012. Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Muda mfupi kabla, Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alitoa taarifa ya maandishi akiishutumu Syria kuiangusha ndege yake ya kijeshi ambayo ilipotea jana Ijumaa.

Mjumbe wa Umoja wa mataifa UN na umoja wa nchi za kiarabu katika mgogoro wa Syria Kofi Annan ametoa wito kwa mamlaka ya dunia kuongeza shinikizo kwa pande zote mbili katika mgogoro wa Syria, ambao wachunguzi wanasema umegharimu maisha ya watu zaidi ya 15,000 tangu Machi 2011.

Aidha maafisa wa shirika la msaada la umoja wa Mataifa wamesema kuwa raia wapatao milioni 1 na nusu nchini Syria kwa sasa wanahitaji msaada,na kuonya kuwa hali nchini humo bado inaendelea kuzorota.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.