Pata taarifa kuu
ATHENS-UGIRIKI

Waziri mkuu mpya wa Ugiriki, Antonis Samaras aahidi kufanya makubwa kwenye Serikali ya muungano

Waziri mkuu mteule wa Ugiriki Antonis Samaras ameahidi kufanya makubwa nchini mwake na kuhakikisha uchumi wa taifa hilo unasimama tena baada ya kupkea mkopo mwingine toka IMF.

Waziri mkuu wa Ugiriki, Antonis Samaras
Waziri mkuu wa Ugiriki, Antonis Samaras Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mara baada ya kula kiapo hapo jana kuchukua majukumu ya uwaziri mkuu, Samaras amesema anafahamu changamoto ambazo zinamkabili mbele yake lakini anaimani kwa ushirikiano na viongozi wengine atafanikisha kuifikisha nchi hiyo kunakotakiwa.

Waziri mkuu anayeondoka Panagiotis Pikrammenos amemwambia Samaras kuwa afahamu ya kwamba anakabiliwa changamoto kubwa mbele yake hasa ya kuboresha maisha ya wananchi wake pamoja na kujenga uaminifu.

Kinachosubiriwa sasa ni kutangazwa kwa baraza jipya la mawaizir ambalo litahusisha viongozi wa chama cha New Democracy na Democratic ambavyo vimekubali kuingia kwenye serikali ya muungano.

Kiongozi wa chama cha Pasok, Evangelos Venizelos amesema kuwa hivi sasa kinachofanyika ni kukamilisha taratibu za uundaji wa serikali pamoja na sera ambazo zitatumiwa na serikali katika kuhakikisha uchumi wa taifa hilo unakua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.