Pata taarifa kuu
ATHENS-UGIRIKI

Antonis Samaras aapishwa rasmi kushika wadhifa wa uwaziri mkuu wa Ugiriki

Antonis Samaras kiongozi wa chama cha New Democracy hatimaye ameapishwa rasmi hii leo kushika wadhifa wa uwaziri mkuu wa Ugiriki mara baada ya kufanikisha mazungumzo na vyama vingine viwili kuhusu uundwaji wa Serikali ya muungano.

Rais wa Ugiriki, Karolos Papoulias (kulia) akipeana mikono na kiongozi wa chma cha New Democracy ambaye ni waziri mkuu wa sasa Antonis Samaras
Rais wa Ugiriki, Karolos Papoulias (kulia) akipeana mikono na kiongozi wa chma cha New Democracy ambaye ni waziri mkuu wa sasa Antonis Samaras © REUTERS/Yorgos Karahalis
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu Samaras anatarajiwa baadae hii leo kutangaza rasmi baraza jipya la mawaziri litakalomsaidia kumaliza mzozo wa kicuhumi ambao umeendelea kuikabili nchi ya Ugiriki.

Kiongozi wa chama cha New Democracy Antonis Samaras ambaye chama chake ndicho kiliibuka mshindi kwenye uchaguzi ulifanyika siku ya Jumapili, alikuwa na mazungumzo yaliingia siku yake ya tatu hii leo na viongozi wenzake wa Pasok na Democratics kabla ya kufikia muafaka.

Akizungumzia kufanikiwa kwa mazungumzo yao, Samaras amesema baada ya mazungumzo ya kina na viongozi wenzake wamefikia makubaliano ya pamoja na kukubali kuunda Serikali ya muungano kusaidia kuitoa nchi ilipo kwenye mdororo wa kiuchumi.

Hivi sasa Samaras anaonana na rais wa nchi hoyo kwaajili ya kumpa taarifa za kufanikiwa kuunda Serikali ya muungano ambapo ataapishwa baadae hii leo kushika wadhifa wa waziri mkuu wa Ugiriki.

Kwa upande wake kiongozi wa chama cha Pasok, Evangelos Venizelos amesema kuwa maazimio waliyoafikiana ni ya muhimu na kwamba sasa kinachobaki ni kukamilisha taratibu za mwishomwisho ambazo zitatoa mwongozo kuhusu uundaji wa sera za serikali ya muungano.

Ijuma hii bune la nchi hiyo linatarajiwa kupiga kura ya kuwa na imani au la na waziri mkuu mpya ambaye ataapihswa na rais baadae hii leo.

tayari viongozi mbalimbali wamepongeza uamuzi uliofikiwa na wanasiasa hao kwa kukubaliana kuunda Serikali ya Umoja wakiamini kuwa watatekeleza matakwa ya Umoja wa Ulaya EU na Shirika la Fedha Duniani IMF ili kuwezesha nchi hiyo kupatiwa mkopo.

Vyama hivyo vitatu vyote vinaunga mkono hatua za ubanaji matumizi ambayo zilitangazwa na serikali iliyotangulia.

Chama pekee ambacho hakitashiriki kwenye Serikali hiyo ni chama cha Syriza abapo kiongozi wake ameapa kutoingia kwenye mazungumzo wa muungano wa Serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.