Pata taarifa kuu
ISLAMABAD-PAKISTAN

Mahakama kuu nchini Pakistan yatangaza kumvua madaraka ya uwaziri mkuu Yusuf Raza Gilani

Mahakama kuu nchini Pakistan imetangaza rasmi kumvua madaraka ya uwaziri mkuu wa nchi hiyo, Yusuf Raza Gilan baada ya kumkuta na hatia ya kuidharau mahakama hiyo kwakushindwa kuanzisha uchunguzi wa masuala ya rushwa dhidi ya rais Asif Ali Zardari.

Waziri mkuu wa Pakistan Yusuf Raza Gilani akipungia mkono wafuasi wake
Waziri mkuu wa Pakistan Yusuf Raza Gilani akipungia mkono wafuasi wake REUTERS/Faisal Mahmood
Matangazo ya kibiashara

Akisoma hukumu hiyo jaji kiongozi Iftikhar Muhammad Chaudhry amesema kuwa waziri mkuu huyo amepoteza nafasi yake toka tarehe 26 ya mwezi wa nne mwaka huu wakati uamuzi wa awali ulipotolewa dhidi yake

Kwenye hukumu hiyo, pia imemtaka rais Zardari kumteua waziri mkuu mpya mapema iwezekanavyo kama njia mojawapo ya kuheshimu uhuru wa mahakama na demokrasia ya nchi hiyo.

Waziri mkuu Gilan alikataa kuiagiza Serikali ya Uswis kufungua tena kesi ya madai ya rushwa dhidi ya rais Zardari kwa kile alichodai kiongozi huyo wa nchi analindwa na katiba ya nchi.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kuwa uamuzi huo ni lazima uazimiwe na bunge jambo ambalo tayari linaonekana kuwa utashindikana kutokana na wabunge wengi kumuunga mkono waziri mkuu Gilani.

Uamuzi huo wa mahakam pia umesema hautatambua maamuzi yoyote ambayo yamefanywa na kiongozi huyo kuanzia mwezi April tarehe 26 jambo ambalo limeelezwa mahakama inataka kuharakisha uchaguzi mkuu kabla ya mwaka 2013 ambapo ndio umepangwa kufanyika uchaguzi mwingine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.