Pata taarifa kuu
ADDIS-ABABA-ETHIOPIA

Ethiopia yatuhumiwa kukiuka haki za binadamu kwenye zoezi la kuwahamisha wananchi wa bonde la Omo

Serikali ya Ethiopia imeshutumiwa vikali na Jumuiya ya kimataifa baada ya kubainika kutumia nguvu kubwa kuwahamisha maelfu ya wananchi kwenye bonde la Omo kwaajili ya mradi wake wa uzalishaji miwa. 

Waziri mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi ambaye nchi yake inatuhumiwa kuwanyanyasa wananchi wa bonde la Omo
Waziri mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi ambaye nchi yake inatuhumiwa kuwanyanyasa wananchi wa bonde la Omo Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na shirika la kutetea haki za binadamu duniani la Human Rights Watch imesema kuwa uchunguzi walioufanya umebaini Serikali ya nchi hiyo kukiuka kwa kiasi kikubwa haki za binadamu wakati wa peresheni hiyo.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa serikali imekuwa ikitumia wanajeshi na Polisi kuwahamisha wananchi hao ambao wengi wao walikuwa wakiishi kwenye bonde hilo kwa miaka zaidi ya mia moja na sasa wanatakiwa kuondoka bila ya kupewa maeneo maalumu.

Ripoti hiyo imeendelea kubainisha kuwa kati kati ya mwaka jana mwezi wa sita, vikosi vya wanajeshi vilitumwa kwenye bonde hilo kwa lengo la kuwatishia maisha wananchi ambao mpaka sasa wamegoma kuhama kwenye eneo hilo.

Serikali ya Ethiopia imeandaa mradi maalumu wa uzalishaji wa Sukari kwa kuweka mashamba makubwa kwenye bonde la Omo ambalo lina maji mengi.

Hatua hiyo ya Ethiopia imekemewa vikali na Umoja wa Mataifa pamoja na wanaharakati wa haki za binadamu ambao wameitaka nchi hiyo kuwalipa fidia wananchi ambao wanatakiwa kuhama kwenye maeneo ya mradi huo.

Hata hivyo serikali ya Ethiopia imekanusha vikali kutumia nguvu kuwahamisha wananchi hao na badala yake imesema kuwa ilishatoa tangazo la muda mrefu kuwataka wananchi hao kutafuta maeneo mengine.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.