Pata taarifa kuu
MYANMAR

50 wapoteza maisha Myanmar tangu kuzuka kwa mapigano ya kidini

Vyombo vya habari vya Myanmar vimeripoti kuuawa kwa watu 50 tangu kuanza kwa machafuko ya kidini huko magharibi mwa Myanmar huku watu 54 wakijeruhiwa mnamo may 28 na june 14.

Raisi wa Myanmar,Thein Sein
Raisi wa Myanmar,Thein Sein
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hiyo haikufafanua kama ilijumuisha idadi ya waislamu 10 walioshambuliwa hadi kufa tarehe 3 june ambapo waumini wa Budha walilipiza kisasi kutokana na ubakaji na mauaji ya mwanamke mmoja ambayo ni chanzo mapigano hayo.

Hata hivyo tayari hali ya tahadhari imeshatangazwa huko Rakhine na matumaini mapya ya majeshi kusaidia kurejesha amani na utulivu baada ya machafuko ambayo yalileta changamoto kubwa kwa utawala wa Myanmar ambao upo katika mageuzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.