Pata taarifa kuu
Hague-ICC

Mwendesha mashataka mkuu mpya wa mahakama ya uhalifu wa kivita ICC Fatou Bensouda aapishwa

Mwendesha Mashtaka Mkuu mpya wa Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC ameapishwa leo mjini Hague kuchukuwa nafasi ya Louis Moreno Ocampo. Fatou  Bensouda, ambae aliewahi kwa wakati mmoja kuhudumu katika serikali ya Gambia kama waziri wa sheria anachukuwa nafasi hiyo na kuwa mwafrika na pia mwanamke wa kwanza kushikilia cheo hicho.

Mwendesha mashtaka mkuu mpya wa mahakama ya uhalifu wa kivita ICC Fatou Bensouda
Mwendesha mashtaka mkuu mpya wa mahakama ya uhalifu wa kivita ICC Fatou Bensouda REUTERS/Bas Czerwinski
Matangazo ya kibiashara

Jukumu la kwanza la kiongozi huyo mpya wa ICC ni kuhakikisha mtoto wa kiongozi wa zamani wa Libya Marehemu kanali Gaddafi Seif Al Islam analetwa katika mahakama hiyo kujibu mashtaka yanayo mkabili ya makosa uhalifu wa kivita, pamoja pia na kuongoza mashtaka yanayomkabili rais wa zamani wa cote d'Ivoire Laurent Gbagbo.

Fatou Bensouda amechukua nafasi ya mtangulizi wake aliestaafu, Luis Moreno Ocampo, ambaye ameongoza mahakama hiyo kwa zaidi ya mwongo mmoja.
Kesi ya rais wa zamani wa Liberia, Charles Taylor, ilisikizwa na mahakama ya Umoja wa mataifa inayosikiliza kesi za waliohusika na vita vya wenyewe kwa wenyewe
Sierra Leone.

Bi Bensouda amekuwa akihudumu kama naibu wa Luis Moreno-Ocampo anayemaliza kazi yake katika mahakama ya ICC. Bensouda sio mgeni kwa mambo ya Hague, uteuzi wake unakuja wakati mfumo wa sheria ya kimataifa unahojiwa sana.
Pia anachukua jukumu hilo wakati kuna mtafaruku katika mahakama hiyo huku maafisa wanne wa mahakama hiyo wakiwa wanazuiliwa nchini Libya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.