Pata taarifa kuu
AU-Ethiopia

Mkutano wa Umoja wa Afrika kufanyika Addis ababa badala ya Lilongwe

Mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika uliopaswa kufanyika nchini Malawi mwezi ujao sasa utafanyika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia. Umuzi huo umechukuliwa baada ya serikali ya Malawi kusema kuwa haitamkaribisha rais wa Sudan Omar Al Bashir nchini humo ambae atahudhuria katika mkutano huo, na itakuwa tayari kumkamata na kumfikisha kwenye mahakama ya uhalifu wa kivita ICC.

Kamishna mkuu wa Umoja wa Afrika Jean Ping
Kamishna mkuu wa Umoja wa Afrika Jean Ping gabonreview.com
Matangazo ya kibiashara

Ferdinand Montcho, ofisaa wa Umoja wa Afrika amethibisha kufanyika kwa mkutano huo mjini Addis Ababa Ethiopia kwenye makao makuu ya Umoja huo, baada ya serikali ya Malawi kushinikizwa na Jumuiya ya kimatifa kumkamata rais Bashir anayetafutwa na Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC kwa tuhuma za mauji katika jimbo la Darfur katika nchi yake.

Rais wa Malawi Joyce Banda alisema mwezi uliopita kuwa alimtaka rais Bashir asihudhurie mkutano huo kwa sababu anataka kuimarisha uhusiano kati ya nchi hiyo na mataifa ya Magharibi hasa yale yanayotoa misaada kwa serikali yake.

Mkutano huo wa Umoja wa Afrika utafanyika kati ya tarehe 9-16 mwezi ujao.
Umoja wa Afrika umeendelea kushutumu mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita  ICC kuwa inaingia maswala ya ndani ya Afrika.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.