Pata taarifa kuu
UGIRIKI

Venizelos katika mtihani wa mwisho wa kujaribu kuunda Serikali ya umoja na kiongozi wa Conservative Antonis Samaras

Kiongozi mkuu wa chama Socialist nchini Ugiriki, Evangelos Venizelos anakutana na kiongozi mkuu wa chama cha Comservatove Antonis Samaras katika mazungumzo mwengine ya awamu ya tatu kujaribu kuunda Serikali ya Umoja.

Antonis Samaras wa kwanza mbele akifuatiwa na Evangelos Venizelos, viongozi hawa wanajaribu kuunda Serikali ya Umoja
Antonis Samaras wa kwanza mbele akifuatiwa na Evangelos Venizelos, viongozi hawa wanajaribu kuunda Serikali ya Umoja Reuters
Matangazo ya kibiashara

Venizelos anatarajiwa kumshawishi Samaras akubali kujiunga na chama chake ili kuunda serikali, mazungumzo ambayo kwa kiasi kikubwa yametabiriwa kuwa yatashindikana kutokana na misimamo tofauti ya vyama hivyo viwili.

Viongozi wa vyama hivyo viwili walikuwa kwenye Serikali ya Umoja wa kitaifa mpaka siku ya Jumapili mara baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu ambapo mara baada ya hapo kila chama kimekuwa kwenye harakati za kujaribu kutafuta uungwaji mkono ili kuwezesha kuunda Serikali.

Mazungumzo hayo yanafanyika baada ya uchaguzi huo wa wabunge kumalizika na matokeo kuonyesha hakuna chama ambacho kilikuwa kimefikisha nusu ya kura ambazo zingewezesha chama kimoja kuunda Serikali.

Wananchi wengi walioshiriki zoezi la upigaji kura wameelezwa kufanya hivyo kutokana na kuchukizwa na hatua ambazo zimechukuliwa na serikali za mpango wake wa kubana matumizi ambao umeshuhudia wafanyakazi wengi nchini humo wakipoteza ajira.

endapo mazungumzo kati ya viongozi hawa wawili yatashindikana basi ni wazi kuwa rais wa nchi hiyo atatumia nguvu aliyonayo kikatiba kuwaagiza viongozi hao kwa mara ya mwisho kutengeneza Serikali ya Umoja wa kitaifa.

Chama cha Pasok kilijikuta kikipata pigo kwenye uchaguzi wa siku ya Jumapili baada ya kuibuka mshindi wa tatu baada ya kujikusanyia vito vya ubunge 41 kati ya 300.

Chama cha Samaras ndicho ambacho kimeonekana kuchukua viti vingi baada ya kujinyakulia viti 108 vya ubunge.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.