Pata taarifa kuu
UGIRIKI

Kiongozi wa chama cha Pasok nchini Ugiriki, Evangelos Venizelos aendelea na juhudi zakutaka kuunda Serikali ya Umoja

Kiongozi wa chama Pasok ambacho kilichokuwa kinaunda Serikali ya umoja nchini Ugiriki, Evangelos Venizelos ameanza harakati za kuvishawishi vyama vingine vya upinzani kukubali kuunda nae Serikali ya umoja. 

Evangelos Venizelos kiongozi wa chama cha Pasok ambaye anajaribu kuunda Serikali ya Umoja
Evangelos Venizelos kiongozi wa chama cha Pasok ambaye anajaribu kuunda Serikali ya Umoja Reuters
Matangazo ya kibiashara

Awali kiongozi huyo alishindwa kufikia muafaka na viongozi wa vyama vya New Democracy na wale wa chama cha Syriza ambapo mazungumzo yao yalivunjika katikati kabla hawajakubaliana muundo wa Serikali utakuwaje.

Mara baada ya mazungumzo ya awali kushindikana, Venizelos atakutana na rais wa nchi hiyo Karolos Papoulias kwa lengo la kutaka kupata idhini ya kujaribu kuunda Serikali ya umoja ambayo tayari chama cha Syriza kimepinga.

Hatua ya Venizelos inakuwa jitihada za mara ya tatu mfululizo kujaribu kufanya mazungumzo na upinzani kujaribu kuwashawishi wakubali waunde Serikali ambayo itaendelea kuunga mkono mpango uliopitishwa na Serikali wa kubana matumizi.

Chini ya mpango wa kuinusuru nchi hiyo na mdororo wa kiuchumi Serikali moya itakayoundwa itakuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa bunge la nchi hiyo linapitisha mpango mwingine wa kubana matumizi utakaowezesha nchi hiyo kupatiwa mkopo wa zaidi ya Euro bilioni 14.

Hapo jana mazungumzo mengine yaligonga mwamba kati ya viongozi wa chama cha Syriza ambao walikuwa wanajaribu kuunganisha nguvu na vyama vingine ambavyo vinapinga ubanaji matumizi mazungumzo ambayo nayo yameonekana kutozaa matunda.

Chama hicho kimekuwa mstari wa mbele kupinga juhudi za Serikali iliyopita ya kuendelea na mpango wa kubana matumizi mpango ambao wamesema ndio ulioitumbukiza nchi hiyo kwenye matatizo ya uchumi iliyonayo.

Kuchelewa kuundwa kwa serikali mpya nchini Ugiriki kumeendelea kuzusha hofu kwa nchi hiyo kupatiwa mkopo wa kunusuru uchumi wake ili kuendelea na juhudi za kufufa uchumi ambazo endapo Serikali isipopatikana mapema basi baadhi ya mambo ambayo yalikuwa yameanza kufanyiwa kazi yatasimama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.