Pata taarifa kuu
MALAWI

Shughuli nyingi za biashara zasimama nchini Malawi hii leo kufuatia kushushwa thamani ya Kwacha dhidi ya Dola

Serikali ya Malawi imeamua kupunguza thamani ya pesa yake kwa asilimi thelathini na nne dhidi ya dola na kuifanya kwacha kuanguka lengo likiwa ni kutekeleza matakwa ya Shirika la Fedha Duniani IMF. 

Rais wa Malawi Joyce Banda
Rais wa Malawi Joyce Banda Reuters
Matangazo ya kibiashara

Benki Kuu ya Malawi imetoa tangazo la kuishusha thamani kwacha na sasa dola moja itakuwa inabadilisha kwa kwacha mia mbili hamsini badala ya ilivyokuwa Ijumaa ambapo dola moja ilikuwa sawa na kwacha mia moja na sitini na sita.

Serikali ya Malawi imefikia uamuzi huo kwa ajili ya kuwaridhisha wahisani na hatimaye waweze kupata msaada baada ya utawala wa Rais Bingu wa Mutharika kukatisha uhusiano na IMF kupinga hatua ya kushusha thamani fedha yao.

Awali nchi ya Uingereza ilitangaza kusitisha kuipatia misaada nchi hiyo pamoja na kusitisha kuchangia bajeti ya nchi hiyo kwakile ilichoeleza ni sera mbovu za serikali ya rais Bingu wa Mutharika aliyesitisha uhusiano wa kibalozi na nchi ya Uingereza.

Shirika la Fedha duniani IMF liliita serikali ya Malawi kushusha thamani ya fedha yake kama njia mojawapo ya kuabiliana na tatizo la mdororo wa kiuchumi ambao ulikuwa umeanza kuathiri wananchi wengi.

Upinzani mara kadhaa ulishiriki maandamano ya nchi nzima kupinga hatua ya serikali kusistisha uhusiano na mataifa ya magharibi kwakile walichodai kufanya hivyo ni kutaka kuwapa umasikini wananchi.

Lakini wakati serikali hiyo ikitangaza kushusha thamani ya fedha yake, hii leo biashara nyingi zimeonekana kufungwa kama njia moja wapo ya kuonesha kuchukizwa kwao na hatua ambayo imetangazwa na rais Joyce Banda.

Wachambuzi wa masuala siasa wanaona kuwa uamuzi wa rais Banda umeshinikizwa kisiasa zaidi na wala haukuwa ni matakwa ya wananchi wengi wa Malawi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.