Pata taarifa kuu
UGIRIKI

Chama cha mrengo wa kushoto nchini Ugiriki mbioni kuunda Serikali inayopinga ubanaji matumizi

Kiongozi mkuu wa chama cha mrengo wa kushoto nchini Ugiriki, Alexis Tsipras ameanza mazungumzo na vyama vingine vya upinzani kujaribu kuunda serikali ambayo inapinga hatua ya ubanaji matumizi. 

Alexis Tsipras kiongozi wa chama cha mrengo wa kushoto nchini Ugiriki
Alexis Tsipras kiongozi wa chama cha mrengo wa kushoto nchini Ugiriki Reuters
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa kiongozi huyo kuamua kutafuta uungwaji mkono toka kwa vyama vya upinzani vinavyopinga serikali ya awali iliyokubali hatua za ubanaji wa matumizi ili kupatiwa mkopo imekuja baada ya vyama viwili vilivyokuwa vinaunda serikali kushindwa kufikia makubaliano ya kuunda serikali ya pamoja.

Viongozi wa vyama vya New Democracy na kile cha Pasok hapo jana walishindwa kuafikiana kuhusu uundwaji wa serikali mpya ya umoja wa kitaifa baada ya kutokea kutoelewana kuhusu muundo wa serikali.

Wananchi wa Ugiriki waliopiga kura siku ya Jumapili waliamua kupigia kura vyama vingine vya upinzani ambavyo vilikuwa mstari wa mbele kupinga hatua ya serikali ya kubana matumizi hatua iliyoelezwa ni kuchukizwa na iliyokuwa serikali ya umoja wa kitaifa iliyopitisha hatua za ubanaji wa matumizi.

Nchi hiyo iliamua kukubali mpango wa kubana matumizi kwa lengo la kupatiwa msaada wa fedha wa zaidi ya Euro bilioni 240, fedha ambazo zingetumika kunusuru uchumi wa taifa hilo.

Hapo jana kansela wa Ujerumani Angela Markel amenukuliwa akiwataka viongozi na wananchi wa Ugiriki kukubalina na masharti ya ubanaji wa matumizi ambayo ni muhimu kwaajili ya kuinusuru nchi hiyo.

Tayari hofu imeanza kutanda kwenye baadhi ya nchi wananchama wa Umoja huo ambao wanaona endapo Ugiriki ikishindwa kuwa na serikali itakayokubali kubana matumizi basi hali ya uchumi kwenye mataifa mengine ya Ulaya itaendelea kuwa mbaya zaidi.

Nchi ya Ugiriki ililazimika kupunguza wafanyakazi wa umma na kupitisha bajeti ya ubanaji wa matumizi ya Serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.