Pata taarifa kuu
MYANMAR

Katibu Mkuu wa UN Ban aiagiza Serikali ya Myanmar kumaliza umwagaji wa damu Kaskazini mwa Nchi hiyo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon ameitaka serikali ya Myanmar kumaliza umwagaji wa damu ambao unaendelea kushuhudiwa Kaskazini mwa nchi hiyo huku akimsihi Rais Thein Sein na Kiongozi wa Upinzani Aung San Suu Kyi kuzungumza kwa lengo la kufikia suluhu ya mgongano wa kiapo cha bunge uliopo.

Rais wa Myanmar Thein Sein akiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon walipokutana kwenye makazi ya Rais
Rais wa Myanmar Thein Sein akiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon walipokutana kwenye makazi ya Rais
Matangazo ya kibiashara

Ban ambaye amekuwa ni mtu wa kwanza raia wa kigeni kuhutubia Bunge la Mynamar tangu serikali ya kiraia iingie madarakani kuchukua nafasi ya Utawala wa Kijeshi ambao ulikaa madarakani kwa miongo miwili na kutajwa kwa kiasi kikubwa kuvuruga demokrasia katika nchi hiyo.

Katibu Mkuu Ban kwenye hotuba yake kwa wabunge wa Bunge la Myanmar amezitaka nchi za Magharibi kuiondolea vikwanzo nchi hiyo kutokana na hatua ambazo wamepiga katika kuhakikisha demokrasiainarejea katika nchi hiyo.

Ban bila ya kung'ata maneno ameitaka serikali ya Myanmar kuhakikisha inamaliza umwagaji wa damu ambao unaendelea kutamalaki katika Jimbo la Kachin na kusema huu ni wakati wa kurejea utulivu katika eneo hilo.

Kiongozi huyo anayeongoza Taasisi kubwa zaidi katika ngazi ya kimataifa amesema bila ya kumaliza umwagaji katika nchi hiyo haitoonekana kwenye jumuiya ya kimataifa kama kweli imefanikiwa kurejesha utawala wa kidemokrasia ambao umekuwa ukililiwa na wengi.

Katibu Mkuu Ban amesema katika kuunga mkono serikali ya Myanmar iweze kutekeleza kwa dhati urejeshaji wa demokrasia ni lazima Mataifa ya Magharibi yawe mstari wa mbele katika kuhakikisha yanaondoa vikwazo kwa taifa hilo.

Ziara hii ya Katibu Mkuu Ban nchini Myanmar inakuja kipindi hiki ambacho Kiongozi wa Chama Kikuu Cha Upinzani cha NLD Aung San Suu Kyi akiridhia hatua ya kula kiapo na kuwa mbunge wa nchi hiyo baada ya kukaa juma moja lililopita.

Tangu Utawala wa kiraia uingie madarakani nchini Myanmar mwaka mmoja uliopita Viongozi wengi wamezuru katika nchi hiyo na kuchangia kuondolewa kwa vikwazo vilivyowekwa wakati Jeshi likishika hatamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.