Pata taarifa kuu
Pakistani- Mahakama

Waziri mkuu wa Pakistani Yousuf Raza Gilani akutwa na hatia

Waziri mkuu wa Pakistan Yousuf Raza Gilani amehukumiwa na mahakama nchini baada ya kukutwa na hatia ya kutoheshimu mahakama. Hatuwa hii inaeweza kumpelekea waziri huyo akapoteza kiti chake.

waziri mkuu wa Pakistan Yusuf Raza Gilani  26/04/2012.
waziri mkuu wa Pakistan Yusuf Raza Gilani 26/04/2012. REUTERS/Faisal Mahmood
Matangazo ya kibiashara

Gilani alihukumiwa katika mahakama na kuwekwa kizuizini kwa masaa kadhaa kabla ya kuachiwa huru muda mfupi baadaye aliibuka huku akitabasamu na akipunga mkono kwa wafuasi wake.

Jaji mkuu wa mahakama Nasir ul Mulik akitowa uamuzi huo amesema waziri mkuu Raza Gilani amepatikana na hatia ya dharau kwa makusudi dhidi ya uongozi wa Mahakama Kuu.

Waziri mkuu huyo wa Pakistani Yousef Raza Gilani amesema atakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ya rufaa nchini nchini humo kumkuta na kosa la kukataa kumfungulia kesi ya Ufisadi rais wa nchi hiyo Asif Ali Zardari.

Wakili wa waziri huyo mkuu Aitzaz Ahsan amesema atawasilisha rifaa hiyo baada ya mteja wakr kupatikana na kosa hilo la kupuuza agizo la mahakama la kumfungulia kesi za ufisadi rais Zardari.

Gilani amekuwa akikanusha tuhma dhidi yake ya kukataa kufungia kesi dhidi ya Rais Zardari anayetuhumiwa kuhusika ka kashfa za kushiriki katika biashara haramu za fedha na benki nchini Swiserland.

Wadadisi wa mambo wanasema nchini Pakistani wanasema kesi hiyo inaingiliwa mno kutokana na mgogoro unaoendelea kati ya mahakama ambayo wengi wanaamini inaungwa mkono mno na majeshi dhidi ya serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.