Pata taarifa kuu
PAKISTAN

Watu 127 wahofiwa kupoteza maisha katika ajali ya ndege,Pakistan

Serikali ya Pakistan imeanza uchunguzi kufuatilia ajali ya ndege ya abiria iliyolipuka wakati ikijaribu kutua ikiwa na abiria 127 ambao wanahofiwa kupoteza maisha.

Nchi ya Pakistan kama inavyoonekana katika ramani
Nchi ya Pakistan kama inavyoonekana katika ramani Infoplease.com
Matangazo ya kibiashara

Ndege hiyo ilipata ajali jirani na kijiji nje kidogo ya mji mkuu wa islamabad siku ya ijumaa ilipokuwa ikikaribia uwanja wa kimataifa mjini humo.

Taarifa kutoka kwa shirika la ndege hiyo imesema abiria walikuwa 121 wakiwemo watoto 11 pamoja na wahudumu 6.

Afisa wa polisi Fazle Akbar akiwa katika eneo la ajali ameliambia shirika la habari la ufaransa kuwa hakuna matumaini ya kupata manusura labda kwa muujiza kwa kuwa ndege hiyo imeungua vibaya.

Hata hivyo juhudi za uokozi zimefanikiwa kupatikana kwa miili 110 kiongozi wa jeshi Safraz Ali amethibitisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.