Pata taarifa kuu
SYRIA-UFARANSA

Nchi marafiki wa Syria wasema mpango wa Annan kuhusu suluhu nchini Syria ni tumaini la Mwisho

Mataifa yenye nguvu duniani yameendelea kuishinikiza serikali ya Syria inayoongozwa na Rais Bashar Al Assad yameendelea kuitaka kuheshimu mapendekeo sita ya mpatanishi wa Mgogoro huo Kofi Annan yakiamini hiyo ndiyo suluhu ya mwisho ya kusitisha umwagaji wa damu. 

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Alain Juppe akiteta jambo na waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Alain Juppe akiteta jambo na waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton REUTERS/Jacquelyn Martin/Pool
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo umefikiwa wakati Mataifa hayo yalipokutana Paris na kuzileta pamoja nchi nne ambazo ni Ufaransa, Marekani, Saudi Arabia na Qatar zikiendelea kujadili ni kwa namna gani mapendekezo ya Annan yanatekelezwa kwa wakati.

Mwenyeji wa Mkutano huo uliopewa jina la Marafiki wa Syria ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Alain Juppe alizitaka nchi washirika wa serikali ya Damascus ikiwepo China na Urusi kuungana nao ili kuendelea kushinikiza kutekelezwa kwa mapendekezo sita ya Annan.

Hatua ambayo ilionekana kuungwa mkono na Viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo akiwemo Mkuu wa Sera za Kimataifa kutoka Umoja wa Ulaya EU Catherine Ashton ambaye amesima muda umefika ya kufanya shughuli zao kwa vitendo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton naye hakukaa kimya badala yake aliendelea kuishinikiza serikali ya Damascus kuhakikisha mapendekezo hayo sita yanaheshimiwa na kutekelezwa.

Waziri Clinton bila ya kusita amesema tumaini la mwisho la kusitishwa kwa machafuko yanayoendelea nchini Syria ni kutekelezwa kwa mapendekezo sita ya Mpatanishi Kofi Annan.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki-moon ametaka ongezeko la waangalizi nchini Syria ili wafikie mia tatu lakini akikiri watu hao wanakabiliwa na kazi ngumu sana kwa sasa.

Katibu Mkuu Ban amesema wanachotaka kwa sasa ni kuhakikishiwa na serikali ya Damascus watawapatia ulinzi wa kutosha pamoja na usafiri wa uhakika waangalizi hao ili waweze kuendesha zoezi lao kwa mafanikio licha ya kukabiliwa na hatari ya usalama wa maisha yake.

Mapigano ya mara kwa mara ndiyo yanaonekana hatari ambao inawakabili waangalizi wa Umoja wa Mataifa UN ambao wanajukumu la kukagua na kujionea hali halisi ilivyo kutokana na uwepo wa madai ya mashambulizi.

Kwa upande wake Mkuu wa Waangalizi hao Kanali Ahmed Himmiche amesema siku ya leo ijumaa watapumzika ili kujiepusha kuingia kwenye mlengo wa machafuko na maandamano ambayo yameandaliwa hii leo.

Machafuko nchini Syria yamedumu kwa miezi kumi na tatu huku takwimu za mwisho za Umoja wa Mataifa UN kupitia Tume ya Haki za Binadamu zinaonesha zaidi ya watu elfu tis a wamepoteza maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.