Pata taarifa kuu
MAREKANI-AFGHANISTAN-NATO

Marekani walaani vitendo vya udhalilishaji vinavyofanywa na wanajeshi wake nchini Afghanistan

Serikali ya Marekani imelazimika kulaani kitendo cha wanajeshi wa nchi hiyo waliopo nchini Afghanistan kupiga picha na maiti za watuhumiwa wa kujitoa mhanga waliotekeleza mashambulizi katika nchi hiyo. 

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Leon Panetta
Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Leon Panetta Reuters
Matangazo ya kibiashara

Picha hizo zimechapishwa katika Gazeti la Los Angeles Times kwa mara ya kwanza ukiwa ni muendelezo wa vitendo vya utovu wa nidhamu vinavyofanywa na wanajeshi hao tangu waingie nchini Afghanistan kitu kilicholaaniwa vikali na Katibu Mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Leon Panetta akihudhuria Mkutano wa NATO uliofanyika Brussels nchini Ubelgiji amesema wamesikitisha na kitendo hicho ambacho hakiungwi mkono na serikali ya taifa hilo.

Picha hizo zimechapishwa wakati ambapo mwaka jana picha nyingine za video zilitolewa zikiwaonyesha wanajeshi wa Marekani wakiwamwagia haja ndogo wapiganaji wa Taliban ambao waliuawa kwenye mashambulizi.

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa picha hizo mpya huenda zikaamsha hasira zaidi kwa wananchi wa Afghanistan ambao wamekuwa wakilaani matendo ambayo yanafanywa na wanajeshi hao kwa raia wa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.