Pata taarifa kuu
SYRIA

Umoja wa nchi za Kiarabu wataka juhudi zaidi kuchukuliwa kumaliza mzozo wa Syria

Wanachama wa Umoja wa Nchi za Kiarabu pamoja na Mpatanishi wa Kimataifa wa Mgogoro wa Syria Kofi Annan wamekutana na kwa kauli moja wameitaka serikali ya Damascus kutekeleza mapendekezo ya kusitisha mapigano wanayodaia bado haijatekelezwa. 

Waangalizi wa Umoja wa Mataifa ambao wako nchini Syria kutathimini hali ya mambo
Waangalizi wa Umoja wa Mataifa ambao wako nchini Syria kutathimini hali ya mambo REUTERS/Khaled al- Hariri
Matangazo ya kibiashara

Tamko hilo linakuja wakati huu Waangalizi wa Umoja wa Mataifa UN waliopo nchini Syria wakikiri wanakabiliwa na kibarua kigumu wakati huu ambapo watu saba wakipoteza maisha katika machafuko mapya yaliyodumu kwa siku sita sasa.

Kiongozi wa Msafara wa Waangalizi hao wenye lengo la kujionea hali halisi ilivyo Kanali Ahmed Himmiche amekiri bado kuna kazi kubwa huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Alain Juppe akisema wanataka waangalizi hao wawe huru.

Kuwasili kwa waangalizi hao wa Umoja wa Mataifa kumesaidia kwa kiasi kikubwa kusitishwa kwa mapigano kati ya majeshi ya Syria na wanjeshi huru wa Syria hatua mabyo imeelezwa huenda ikazaa matunda katika kumaliza mzozo nchini humo.

Kumeripotiwa mapigano kwenye baadhi ya miji ambapo pande zote mbili zimekuwa zikishutumiana kumshambulia mwenzie hatua ambayo inaelezwa itachochea machafuko mengine mapya.

Hapo jana serikali ya Syria ilitoa taarifa ikidai kuwa wanajeshi wa jeshi huru la Syria wamekuwa wakiwashambulia wanajeshi wa serikali ambao wameanza kuodnoak kwenye baadhi ya miji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.