Pata taarifa kuu
MYANMAR

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Myanmar Aung San Suu Kyi apanga kufanya ziara ya kwanza barani Ulaya

Baada ya kuhudumu kifungo cha ndani kwa zaidi ya miaka ishirini, kiongozi mkuu wa upinzani nchiniu Myanmar Aung San Suu Kyi, ametangaza kufanya ziara ya kwanza barani ulaya mwezi June mwaka huu. 

Waziri mkuu wa Uingereza akiwa na Aung San Suu Kyi wakati alipofanya zaiara nchini Myanmar
Waziri mkuu wa Uingereza akiwa na Aung San Suu Kyi wakati alipofanya zaiara nchini Myanmar Reuters
Matangazo ya kibiashara

Suu Kyi amethibitisha kupanga kufanya ziara hizo nchini Norway na Uingereza kama hatua zake za awali za kutaka kuzishawishi jumuiya za kimataifa kuendelea kuiondolewa vikwazo nchi hiyo.

Mshindi huyo wa tuzo la Nobel mwaka 1991 tayari ameshatuma maombi ya kupatiwa pasi ya kusafiria kwa maofisa wa ubalozi wa nchi hizo mbili ambapo mpaka sasa bado hayajajibiwa ingawa kuna uwezekano mkubwa wa kupatiwa pasi hizo.

Akiwa nchini Norway kiongozi huyo anatarajiwa kuhutubia kongamano katika uwanja wa Oslo City ambapo pamoja na mambo mengine atatoa historia ya maisha yake wakati akiwa mfungwa kwa miaka 22.

Mwezi mmoja uliopita waziri mkuu wa Uingereza David Cameroon alifanya ziara nchini Myanmar na kukutana na kiongozi huyo ambapo ziara kama hiyo iliwahi kufanywa pia na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton.

Umoja wa Ulaya ikiwemo Marekani tayari zimatangaza kuanza kuondoa baadhi ya vikwazo ambavyo nchi hiyo ilikuwa imewekewa toka utawala wa kijeshi ulirejesha madaraka kwa serikali ya kiraia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.