Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-KABUL

Usalama warejea mjini Kabul baada ya saa 17 za mapigano

Serikali mjini Kabul nchini Afghanistan imetangaza kufanikiwa kuwaua wapiganaji thelathini na sita toka kundi la wanamgambo wa Taliban waliokuwa wameanzisha mapigano kwenye mji mkuu wa nchi hiyo. 

Moja ya jengo ambalo wanamgambo wa Taliban walikuwa wakilitumia kutekeleza mashambulizi yao
Moja ya jengo ambalo wanamgambo wa Taliban walikuwa wakilitumia kutekeleza mashambulizi yao Reuters
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya ndani wa Afghanistan, Bismillah Mohammadi amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kudai kuwa wanamgambo hao waliuawa wakati wakikabilina na polisi kwa kushirikiana na majeshi ya kigeni nchini humo.

Wanamgambo wa Taliban hapo jana walianzisha mashambulizi yakushtukiza yaliyolenga ofisi za Serikali, vituo vya polisi, kambi za majeshi ya kigeni mjini Kabul pamoja na balozi za mataifa ambayo yanamajeshi nchini humo.

Waziri huyo wa mambo ya ndani amesema kuwa wanajeshi wa NATO walifanikiwa kumtia mbaroni mwanamgambo mmoja wa Taliban aliyekuwa akitaka kujitoa muhanga kwenye ofisi zake mjini Kabul akiwa kwenye mji wa Jalalabad.

Mkuu wa polisi mjini Kabul, Mohammad Ayoub Salagi ameongeza kuwa zaidi ya mateka arobaini waliokuwa wanashikiliwa na wanamgambo hao kwenye jengo moja jirani na ukumbi wa bunge walifanikiwa kuwaokoa majira ya usiku baada ya kuzima jaribio la wanamgambo hao.

Tayari kundi la Taliban limekiri wapiganaji wake kuhusika kwenye mashambulizi hayo na kudai kuwa linajiandaa kufanya mashambulizi mengine kama hayo hivi karibuni.

Mashambulizi ya hapo jana yameelezwa kuwa mashambulizi yaliyopangwa kuwahi kufanywa na kundi hilo katika kipindi cha miaka kumi toka uvamizi wa majeshi ya kigeni yalioingia nchini humo kupambana na wanamgambo hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.