Pata taarifa kuu
OSLO-NORWAY

Mtuhumiwa wa ugaidi nchini Norway, Anders Breivik asema hana hatia

Mtuhumiwa wa mauaji ya watu 77 nchini Norway Anders Behring Breivik hii leo amepandishwa kizimbani kujibu mashtaka yanayomkabili huku akikana mashtaka yanayomkabili. 

Mtuhumiwa wa ugaidi nchini Norway Anders Breivik akipunga mkono wakati akiingia mahakamani
Mtuhumiwa wa ugaidi nchini Norway Anders Breivik akipunga mkono wakati akiingia mahakamani Reuters
Matangazo ya kibiashara

Akiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi Breivik aliingia mahakamani hapo akiwa hana wasi wasi akiongozwa na wakili wake huku akionekana akitabasamu muda wote wakati kesi yake ikiendelea.

Mara baada ya kuulizwa na jaji kama anakubali au kukataa mashtaka yaliyoko mbele yake, Breivik alijibu anakiri kuhusika na tukio hilo lakini yeye sio gaidi kama mwendesha mashtaka wa serikali alivyothibitisha mahakamani.

Katika maongezi yake, Breivik amesema kuwa haitambui mahakama inayosikiliza kesi hiyo akidai kuwa inaongozwa kisiasa na kwamba wamepanga kumkuta na hatia ya makosa aliyotekeleza.

Mtuhumiwa huyo amekiri kutekeleza shambulio la bomu la gari mjini Oslo kwenye ofisi za serikali na kuua watu 8 na kujeruhi wengine 69 kabla ya kuelekea kwenye visiwa vya Utoya na kutekeleza mauaji mengine.

Kumekuwa na mvutano kuhusu utimamu wa mtuhumiwa huyo huku uchunguzi wa awali ukionesha kuwa Breivik alikuwa hana akili timamu wakati akitekeleza mauaji yale ambapo uchunguzi wa mwezi mmoja uliopita ulipinga Breivik kutokuwa na akili timamu.

Kesi hiyo inaendeshwa huku wataalamu wa masuala ya akili wakisikiliza kesi hiyo inavyoendeshwa kwa lengo la kutaka kubaini kama kweli Breivik ana akili timamu au la.

Mwendesha mashtaka wa serikali hii leo ameonesha mkanda wa video ukimuonesha Brievik akitekeleza shambulio la mjini Oslo na lile la kwenye visiwa vya Utoya.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.