Pata taarifa kuu
SRI LANKA

Onyo la kutokea Tsunami kwenye Pwani ya Bahari ya Hindi latolewa wakati huu ambapo Sri Lanka ikiwa muathirika wa kwanza

Onyo la kutokea kwa Tetemeko la Nchini ya Bahari maarufu kama Tsunami kwenye Visiwa vilivyopo ndani ya Bahari ya Hindi limetolewa baada ya Kisiwa cha Sri Lanka kupigwa na tetemeko hilo kitu ambacho kimeanza kuibua hisia za kurejea kwa tukio kama hilo lililotokea mwaka elfu mbili na nne. Serikali ya Sri Lanka imewataka wananchi wanaokaa kwenye eneo la Pwani kuondoka mara moja na kuahamia maeneo ya Bara ili kuepukana na madhara ya mawimbi makubwa na makali ambayo yameanza kushuhudiwa katika nchi hiyo kwa sasa.

Wananchi wa Indonesia wakikimbia makazi yao baada ya kutolewa onyo la kutokea kwa Tsunami kwenye Pwani ya Bahari ya Hindi
Wananchi wa Indonesia wakikimbia makazi yao baada ya kutolewa onyo la kutokea kwa Tsunami kwenye Pwani ya Bahari ya Hindi AFP
Matangazo ya kibiashara

Taasisi inayoshughulikia majanga nchini Sri Lanka imeanza kusimamia zoezi la kuanza kuwaondoa wakazi wa eneo la Trincomalee ambalo linatajwa kuwa la kwanza kupata madhara ya tetemeko hilo.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Sarath Kumara amesema maeneo ya Mashariki na Kusini mwa Pwani ya kisiwa hicho ni hatari sana kipindi hiki na hivyo akatoa wito kwa wakazi hao kuhamia maeneo salama kuepuka kadhia inayoweza kutokea.

Tetemeko hilo la chini ya bahari maarufu kama Tsunami limetajwa kuwa na kipimo cha nane nukta saba katika vipimo vya matetemeko badala ya nane nukta tisa kama ambavyo iliripotiwa awali.

Kitengo cha Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa nchini Sri Lanka imesema kuwa kuna kila dalili ya kutokea Tsunami katika nchi hiyo baada ya jirani zao Indonesia kushuhudia wakipigwa na tetemeko la ardhi.

Takwimu rasmi za Tsunami ya mwaka elfu mbili na nne nchini Sri Lanka zinaonesha kuwa watu elfu thelathini walipoteza maisha huku madhara mengine makubwa yakishuhudiwa katika nchi hiyo.

Wataalam wa Masuala ya Matetemeko wamesema kuna kila dalili nchi za Australia, Pakistan, Somalia, Tanzania, Kenya, Madagascar na nchi nyingine ambazo zipo kwenye eneo la pwani ya Bahari ya Hindi zinaweza kukutwa na Tsunami hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.