Pata taarifa kuu
SRI LANKA-THAILAND-INDONESIA

Onyo la kutokea kwa Tsunami kwenye Pwani ya Bahari ya Hindi laondolewa baada ya kutokea tetemeko la ardhi huko Sumatra

Onyo la kutokea kwa tetemeko la chini ya bahari maarufu kama Tsunami lililokuwa linatarajiwa kupiga eneo la Pwani ya Bahari ya Hindi limeondolewa baada ya tetemeko lenye kipimo cha nane nukta sita kupiga kisiwa cha Sumatra.Onyo hilo limeondolewa katika nchi za Indonesia, india na Thailand ambazo zilikuwa zinatajwa kuwa kwenye hatari kubwa zaidi za kukumbwa na Tsunami lakini wataalamu wa masuala ya miamba wamesema kiticho hicho hakipo tena.

Wakazi wa Indonesia hasa eneo la Banda Aceh wakiyahama makazi yao kupisha tetemeko la chini ya bahari Tsunami lililokuwa linatarajiwa kutokea
Wakazi wa Indonesia hasa eneo la Banda Aceh wakiyahama makazi yao kupisha tetemeko la chini ya bahari Tsunami lililokuwa linatarajiwa kutokea Reuters
Matangazo ya kibiashara

Ahueni imekuja baada ya kutokea kwa tetemeko hilo nchini Indonesia kitu ambacho kilizifanya Mamlaka za Hali ya hewa nchini Sri Lanka kutangaza nchi hiyo kutopigwa tena na tetemeko hilo la chini ya bahari maarufu kama Tsunami.

Waatalam wa masuala ya miamba nchini marekani katika eneo la Hawaii wameondoa kitisho hicho na kusema nchi kadhaa ambazo zilitajwa hapo mapema kuwa kwenye hatari ya kukumbwa na Tsunami zitakuwa salama.

Taarifa hizi zinakuja wakati nchi nyingi za Afrika Mashariki zikiendelea kutoa tahadhari kwa wananchi wake waliopo kwenye maeneo ya mwambao wa Pwani kuondoka mara moja ili kupisha madhara yanayoweza kutokana na Tsunami hiyo.

Mapema Onyo lilitolewa la kutokea Tsunami kwenye Visiwa vilivyopo ndani ya Bahari ya Hindi kutokana na Kisiwa cha Sri Lanka kupigwa na tetemeko hilo kitu ambacho kilianza kuibua hisia za kurejea kwa tukio kama hilo lililotokea mwaka elfu mbili na nne.

Serikali ya Sri Lanka imewataka wananchi wanaokaa kwenye eneo la Pwani kuondoka mara moja na kuahamia maeneo ya Bara ili kuepukana na madhara ya mawimbi makubwa na makali ambayo yameanza kushuhudiwa katika nchi hiyo kwa sasa.

Taasisi inayoshughulikia majanga nchini Sri Lanka imeanza kusimamia zoezi la kuanza kuwaondoa wakazi wa eneo la Trincomalee ambalo linatajwa kuwa la kwanza kupata madhara ya tetemeko hilo.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Sarath Kumara amesema maeneo ya Mashariki na Kusini mwa Pwani ya kisiwa hicho ni hatari sana kipindi hiki na hivyo akatoa wito kwa wakazi hao kuhamia maeneo salama kuepuka kadhia inayoweza kutokea.

Tetemeko hilo la chini ya bahari maarufu kama Tsunami limetajwa kuwa na kipimo cha nane nukta saba katika vipimo vya matetemeko badala ya nane nukta tisa kama ambavyo iliripotiwa awali.

Kitengo cha Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa nchini Sri Lanka imesema kuwa kuna kila dalili ya kutokea Tsunami katika nchi hiyo baada ya jirani zao Indonesia kushuhudia wakipigwa na tetemeko la ardhi.

Takwimu rasmi za Tsunami ya mwaka elfu mbili na nne nchini Sri Lanka zinaonesha kuwa watu elfu thelathini walipoteza maisha huku madhara mengine makubwa yakishuhudiwa katika nchi hiyo.

Wataalam wa Masuala ya Matetemeko wamesema kuna kila dalili nchi za Australia, Pakistan, Somalia, Madagascar na nchi nyingine ambazo zipo kwenye eneo la pwani ya Bahari ya Hindi zinaweza kukutwa na Tsunami hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.