Pata taarifa kuu
MALI-ECOWAS

Viongozi wa ECOWAS wakutana katika kikao cha dharula kujadili swala la mapinduzi ya kijeshi nchini Mali

Mapinduzi ya kijeshi yaliotokea nchini Mali Machi 22, yaliomuondowa madarakani rais Amadou Toumani Toure, yanaibuwa maswala mengi ndani na nje ya nchi hiyo hususan jamii ya kimataifa. Jamii ya kimataifa imeendelea kulaani tukio hilo huku ikiomba wanajeshi waasi kurejesha utawala wa kikatiba. Viongozi wa mataifa ya jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS wanakutana katika kikao cha dharura jijini Abidjan nchini Côte d’Ivoire ili kuchukuwa maamuzi kuhusu uongozi wa kijeshi ulioipinduwa serikali ya Mali. Wananchi nchi Mali wanasubiri kwa hamu na gamu maamuzi ya jamii ya kimataifa kuhusu uongozi huo wa kijeshi.

Viongozi wa ECOWAS katika kikao cha Abuja, Machi 23.2011
Viongozi wa ECOWAS katika kikao cha Abuja, Machi 23.2011 REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Ufaransa inaunga mkono juhudi za ECOWAS katika kujaribu kurejesha utawala wa kikatiba. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Ufaransa Bernard Valero amesema kuwa Ufaransa inatiwa wasiwasi mkubwa kuhusu hali inayo jiri nchini Mali, hasa kutiwa nguvuni kwa viongozi wa serikali ya Mali, na wanaomba waachiwe huru wakati hali ya rais Toumani Toure haijulikani iko je.

Upande wake nchi Benin inayoongoza kwa sasa Umoja wa Afrika AU imelaani kwa nguvu zote mapinduzi hayo ya kijeshi nchini Mali na imetowa wito kwa wanajeshi walioendesha mapinduzi kurejesha utawala wa kikatiba bila masharti yoyote na kwa sasa ijnamchukulia rais Toumani Toure kwamba ndie kiongozi wa Mali.

Umoja wa Mataifa UN nao pia umelaani vikali mapinduzi hayo na kuwataka wanajeshi walioasi kurejesha mara moja utawala wa kidemokrasia na warejeee kambini.
Kikao cha dharula cha viongozi wa ECOWAS kitatowa maamuzi yatayo tatuwa matatizo ya Mali? Allasane Ouattara rais wa Cote d'Ivoire ambae ndiye kiongozi wa sasa wa ECOWAS
atafaulu kutatuwa changamoto hiyo ya wanajeshi walioendesha mapinduzi? Atapendekeza uingiliaji kijeshi ili kurejesha utawala wa kidemokrasia nchini Mali? Maswala ni mengi ambayo viongozi wa jumuiya ya kiuchumi wa nchi za magharibi wanatakiwa kujibu na wananchi wa Mali wanasubiria lakinipia jamii ya kimataifa.

Mtikisiko wa kisiasa nchini Mali waweza kuhatarisha hali ya usalama katika ukanda mzima na kuyapanguvu makundi ya kigaidi yanayo hujumu katika eneo hilo la Afrika magharibi yakiwemo makundi ya Alqaida. Duru kutoka ikulu ya rais nchini Cote d'Ivoire zaarifu kuwa viongozi wa ECOWAS wataomba utawala wa kidemokrasia urejeshwe na viongozi walioachishwa kazi warejeshwe kwenye nyadhifa zao. Akizungumza kwa njia ya simu na RFI Jean Ping rais wa kamisheniya Umoja wa Afrika AU amekemea mapinduzi hayo huku akisisitiza kwamba uingiliaji kijeshi hautoepukika iwapo itashindikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.