Pata taarifa kuu
MAREKANI-AFGANISTAN

Mwanajeshi wa Marekani anayeshukiwa kutekeleza mauji nchini Afganistan kufikishwa Mahakamani

Mwanajeshi wa Marekani anayeshutumiwa kutekeleza mauaji ya raia 17 wa Afghanistan kwa kuwafwatulia  risasi,  wakiwemo watoto 9 atafunguliwa mashtaka 17 ya mauaji.

Matangazo ya kibiashara

Mshukiwa huyo Sajenti Robert Bales pia atashtakiwa kuhusika na makosa sita ya kujaribu kushambulia na jaribio la kuua.

Bales mwenye Umri wa miaka 38 anatuhumiwa kutekeleza mauaji hayo katika jimbo la Kandahar katikati ya mwezi wa Machi na kwa sasa anazuiliwa katika jela ya kijeshi ya Fort Leavenworth jijini Kansas nchini Marekani.

Mshukiwa huyo atafikishwa katika Mahakama za kijeshi nchini Marekani baadaye siku ya Ijumaa,na ikiwa atapatikana na makosa hayo atapewa adhabu ya kifo.

Wakili wa mshukiwa huyo John Henry Brown anasema hakuna ushahidi dhidi ya mteja wake ,na anaongeza kuwa Bales mwenyewe hajakiri kutekeleza mauji hayo.

Nalo kundi la wanamgambo wa Taliban limesema halina imani na Mahakama nchini Marekani na linahisi kuwa haki haitatendeka,na hivyo linapanga kulipiza kisasi dhidi ya majeshi ya Marekani.

Mauji hayo yamedhoofisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Kabul na Washington, na Afganistan inashinikiza NATO kuyaondoa majeshi yote ya kimataifa nchini humo kabla ya makataa ya mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.