Pata taarifa kuu
Ufaransa-Israel

Maelfu wahudhuria mazishi ya watoto waliouawa kwa kupigwa risasi Kusini mwa Ufaransa,mshukiwa akaribia kujisalimisha

Maelfu ya waombolezaji wamehudhuria mazishi ya watoto watatu na mwalimu wao yaliyofanyika viungani mwa  mji wa Jerusalem nchini Israel,  waliouawa baada ya kupigwa risasi katika shule ya kiyahudi mjini Toulouse Kusini mwa Ufaransa siku ya Jumatatu.

Waombolezaji mjini Jerusalem nchini Israel
Waombolezaji mjini Jerusalem nchini Israel
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa waombolezaji waliohudhuria  katika mazishi hayo ni pamoja na Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Alain Juppe, pamoja na viongozi wengine wa serikali ya Isreal.

Nchini Ufaransa Polisi wameendelea kumzingira mshukiwa wa tukio hilo katika makaazi yake mjini Toulouse na amekuwa akifanya mazungumzo na maafisa hao wa polisi kuhusu kujisalimisha kwake.

Polisi wanasema wanalenga kumkata mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 24 anayetambuliwa kwa jina la Mohammed Merah,ambaye amebainika pia kuwa raia wa Ufaransa mwenye asili ya Algeria, akiwa hai ili afunguliwe mashtaka Mahakamani.

Ndugu wa kiume wa mshukiwa huyo tayari amekamatwa pamoja na watu wengi wanaosadikiwa kuwa karibu naye na wanasaidia polisi kwa uchunguzi zaidi.
 

Rais Nicolas Sarkzoy amesema vitendo vya ugaidi havitaligawa taifa la Ufaransa ambalo lina idadi kubwa ya Waislamu na Wayahudi.

Sarkozy amewataka raia wa Ufaransa kuungana pamoja kushinda ugaidi na kutoa wito kwa raia wake kutolipiza kisasi kwa kile alichokieleza kuwa mauji yaliyotokea hayakuwa ya kidini .

Mshukiwa huyo ambaye amekuwa akihojiwa na maafisa wa ujasusi amekiri kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi la al-Qaeda na amekiri kutenda mauji hayo kuonesha gadhabu zake kuhusu watoto katika mamlaka ya Palestina anaosema  wanaishi katika mazingira magumu.

Waziri wa mambo ya ndani wa Claude Gueant amesema mshukiwa huyo amekuwa akitafutwa na maafisa wa ujasusi wa Ufaransa kwa muda mrefu .

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.