Pata taarifa kuu
SYRIA

Kofi Annan atoa wito kwa umoja wa mataifa kuungana kukomesha machafuko nchini Syria.

Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa mataifa Kofi Annan pamoja na wajumbe wa mataifa ya kiarabu katika umoja wa mataifa kuhusu Syria wametoa wito kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa kuungana ili kusaidia juhudi za upatanishi dhidi ya mgogoro wa Syria.

Kofi Annan se dit prêt à retourner en Syrie pour poursuivre les négociations.
Kofi Annan se dit prêt à retourner en Syrie pour poursuivre les négociations. REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Wito huo wa Annan kwa wajumbe wa baraza hilo kutoka mataifa 15 jana Ijumaa umekuja kufuatia maandamano ya kuipinga serikali kuendelea nchini Syria kutaka majeshi ya kimataifa kuingilia kati mgogoro huo.

Wanaharakati wamesema kuwa jumla ya watu 15 wakiwemo watoto wameuwawa katika vurugu hapo jana katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Aidha wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo imesema kuwa itashirikiana vema na Kofi Annan katika juhudiza kumaliza mgogoro wakati huohuo itapambana kupinga ugaidi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.