Pata taarifa kuu
SYRIA-HOMS

Naibu waziri wa mafuta kwenye Serikali ya Assad atangaza kujiuzulu

Naibu waziri wa mafuta nchini Syria Abdo Hussameddin ametangaza kujiuzulu nafasi yake na kuungana na upinzani nchini humo kushinikiza Serikali ya rais Bashar al-Asad kujiuzulu. 

Homem armado caminha nesta quarta-feira pela cidade destruída de Homs, na Síria.
Homem armado caminha nesta quarta-feira pela cidade destruída de Homs, na Síria. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Licha ya kiongozi huyo kutangaza kujiuzulu bado serikali haijasema chochote kuhusiana na waziri huyo kwa kile kilichoelezwa kuwa hakuna mtu ambaye anaweza kuthibitisha kama picha za viedo zilizoonyeshwa ni za waziri mwenyewe.

Akizungumza kupitia njia ya video ambayo imewekwa kwenye mtandao, naibu waziri Hussameddin amesema kuwa ameamua kujiunga na upinzani kutokana na ukaidi wa serikali katika kushughulikia mgogoro unaoendelea.

Kiongozi huyo ameongeza kuwa kuanzia sasa hatoshiriki mikutano ya chama chake badala yake atashiriki kwenye jitihada za kutaka kufanya mapinduzi ya kidemokrasia nchini humo.

Katika hatua nyingine mkuu wa tume ya misaada ya Umoja wa Mataifa Valerie Amos ameingia kwenye siku ya pili ya ziara yake nchini Syria ambapo anaendelea kukutana na viongozi mbalimbali wa Serikali kujadili hali ilivyo nchini humo.

Hapo jana mara baada ya kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Syria Bi Amos alielekea kwenye mji wa Homs mji ambao umekuwa kwenye mashambulizi kwa majuma kadhaa na kukuta hali imeanza kurejea kama kawaida kutokana na kusitishwa kwa mashambulizi.

Wakati huohuo katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan anatarajiwa kuwasili nchini humo muda wowote kuanzia sasa ambapo atafanya mazungumzo na rais Asad kabla ya kupanga mkutano na upinzani ambao umeunda jeshi huru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.