Pata taarifa kuu
MISRI-SYRIA

Koffi Annan aonya dhidi ya kutumika nguvu za kijeshi nchini Syria

Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan ambaye anatarajiwa kuzuru mjini Damascus siku ya Jumamosi kwa mazungumzo na viongozi wa serikali ya Syria, amesema kuwa kutumia nguvu za kijeshi nchini humo kutfanya hali kuwa mbaya zaidi.

Koffi Annan (kushoto) akiwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon walipkutana hivi karibuni na kumteua kuwa mjumbe kusuluhisha mgogoro wa Syria
Koffi Annan (kushoto) akiwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon walipkutana hivi karibuni na kumteua kuwa mjumbe kusuluhisha mgogoro wa Syria UN Photo/Mark Garten
Matangazo ya kibiashara

Annan ameyasema hayo ikiwa imebaki siku moja tu kwa kiongozi huyo kuzuru mjini Damascus ambako anatarajiwa kukutana na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Syria Walid al-Moualem.

Akizungumza na katibu mkuu wa jumuiya ya Umoja wa Nchi za Kiarabu, Annan amesema kuwa endapo mataifa ya magharibi yataamua kutumia nguvu za kijeshi au kuwasaidia waasi kwa silaha basi mgogoro huenda ukawa mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa toka harakati za mapinduzi zilipoanza.

Annan toka awali wakati wa uteuzi wake amekuwa akisisitiza kuwa yeye ndiye msuluhishi pekee wa mgogoro huo na kwamba asingependa kuona mataifa mengine yanaingilia mazungumzo ambayo anayafanya na pande zinazokinzana.

Akiwa mjini Damascus Annan anatarajiwa kukutana na rais Bashar al-Assad kabla ya kuzungumza na upande wa upinzani ambao umekuwa ukiishutumu serikali ya Assad kwa kufanya mauaji dhidi ya raia.

Ziara ya Annan inakuja wakati ambapo mkuu wa tume ya misaada ya Umoja wa Mataifa bi Valerie Amos akiwa kwenye mji wa Bab Amr ulioko Homs, mji ambao umekuwa kwenye mashambulizi kwa majuma kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.