Pata taarifa kuu
SYRIA-CHINA

China yataka Jumuiya ya Kimataifa kuhakikisha misaada inawafikiwa wananchi wa Syria wanaotahabika

Serikali ya China imeiambia Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ni lazima misaada ya kibinadamu iweze kuwafikia wananchi wanaokabiliwa na hali mbaya nchini Syria na kutaka machafuko yanayoendelea yasitishwe mara moja.

Vifaru vya serikali ambavyo vinatumika kufanya mashambulizi katika Jiji la Homs nchini Syria na kusitisha huduma za kibinadamu kufika kwa wananchi
Vifaru vya serikali ambavyo vinatumika kufanya mashambulizi katika Jiji la Homs nchini Syria na kusitisha huduma za kibinadamu kufika kwa wananchi REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Yang Jiechi amesema kuwa huu ni wakati muafaka wa kudhibiti machafuko yanayoendelea na kuchangia vifo kwa wananchi wasio na hatia katika Jiji la Homs.

Waziri Jiechi ametaka misaada hiyo ya kibinadamu iwafikie wananchi wakati alipofanya mazungumzo kwa njia ya simu ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Nabil Al Arabi katika kuhakikisha wananchi wanasaidiwa.

Kauli ya serikali ya China inakuja wakati huu ambapo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN likianzisha mjadala mkubwa katika kuhakikisha wananchi wa Syria wanapatiwa misaada ya kibinadamu sambamba na kusitishwa kwa machafuko yanayoendelea.

Jiechi amesema kuwa ni lazima Jumuiya ya Kimataifa itengeneze mazingira mazuri yatakayoruhusu misaada kuweza kuwafikia wananchi wa Syriawanaohitaji huduma nyingi za kijamii zikiwemo matibabu.

Haya yanakuja wakati huu ambapo Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa UN ikitoa takwimu mpya ambazo zinaonesha kuwa watu elfu saba na mia sita wamepoteza maisha nchini Syria tangua kuanza kwa machafuko yaliyodumu kwa miezi kumi na moja.

Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa UN Navi Pillay amekiambia kikao cha Umoja huo katika jiji la Geneva nchini Uswiss ambapo pamoja na masuala mengine ametaka kusitishwa kwa mapigano katika nchi hiyo.

Pillay amesema wananchi wengine wanahitaji misaada kwa hiyo kuendelea kufanya mashsmbulizi kunakotekelezwa na Vikosi vitiifu kwa Rais Bashar Al Assad kunachangia watu hao kushindwa kupata huduma.

Mapema Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Alain Juppe alinukuliwa akisema kuwa anaimani Urusi safari hii haitotumia kura yake ya turufu ya veto kupinga azimio ambalo litapendekezwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN dhidi ya Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.