Pata taarifa kuu
SYRIA

Umoja wa Ulaya EU watangaza vikwazo vipya dhidi ya serikali ya Syria inayoongozwa na Rais Bashar Al Assad

Urusi na China zimepata pigo na kuendelea kukosolewa vikali na Marekani kwa kushirikiana na Mataifa mengine nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya EU kutokana na kuiunga mkono serikali ya Rais Bashar Al Assad ambayo inakumbana na vikwazo zaidi. Ukosoaji kwa Urusi na China mataifa rafiki na yaliyomstari wa mbele kuitetea serikali ya Rais Assad kumetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton ambaye amesema kuwa uwezekano mkubwa wa kuibuika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.

Bendera za nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya EU ambao wametangaza vikwazo dhidi ya Serikali ya Syria
Bendera za nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya EU ambao wametangaza vikwazo dhidi ya Serikali ya Syria DR
Matangazo ya kibiashara

Clinton ametoa kauli hiyo kwa kile ambacho anasema kilichoshuhudiwa mwishoni mwa juma ambapo watu mia moja na hamsini walipoteza maisha wakati nchi hiyo iliyoshuhudia upigwaji wa kura ya maamuzi kuruhusu mabadiliko ya katiba.

Mambo haya yanakwenda sambamba na uamuzi wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Ulaya kuamua kushusha vikwazo zaidi dhidi ya Utawala wa Assad kwa kushikilia mali zaidi kutoka Benki Kuu, kuweka vikwazo vya kusafiri kwa watu saba ambao wapo karibu na Rais Assad, kuzuia ndege za mizigo kutua kwenye nchi wanachama pamoja na kudhibiti biasahara ya dhahabu na vito vingine vya thamani.

Uamuzi huo umefikiwa kwa kile ambacho kinatajwa ni kuendelea kuidhibiti serikali ya Rais Assad ili isitishwe umwagaji wa damu ambao unaendelea kushuhudiwa dhidi ya wapinzani wa serikali.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Alain Juppe amesema anataka kuona wale wote wanaochangia hali kuwa mbaya nchini Syria wafikishwe kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita.

Naye Waziri Mkuu wa Qatar Sheikh Hamad Bin Jassem Al Thani amesema huu ni wakati muafaka wa kutoa silaha kwa wapinzani ambao wanapambana na Utawala wa Rais Assad ili waweze kusonga mbele.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Urusi Vladimir Putin amejitokeza na kutetea kwa nguvu zote nchi yake kuendelea kutumia turufu yake ya veto kupinga hatua zozote ambazo zinataka kushukuliwa dhidi ya Rais Assad.

Matukio haya yanatokea wakati huu ambapo zoezi la uhesabuji kura likiendelea nchini Syria ambapo takwimu zinaonesha wananchi wengi walijitokeza kutumia haki yao ya msingi kukubali au kukataa mabadiliko ya katiba na kuruhusu uchaguzi wa vyama vingi ufanyike.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.