Pata taarifa kuu
YEMEN

Ali Abdullah Saleh amekabidhi madaraka rasmi kwa Rais Abdrabuh Hadi

Ali Abdullah Saleh amekabidhi madaraka rasmi kwa Makamu wake Abdrabuh Mansur Hadi ambaye amechaguliwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo baada ya kuongozwa kwa miaka thelathini na tatu na Kiongozi huyo wa zamani.

Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdullah Saleh akikabidhi madaraka kwa mrithi wake katika Makazi ya Rais huko Sanaa
Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdullah Saleh akikabidhi madaraka kwa mrithi wake katika Makazi ya Rais huko Sanaa
Matangazo ya kibiashara

Saleh amekabidhi madaraka kwenye makazi ya rais yaliyopo katika Jiji la Sanaa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya kumaliza machafuko na hatimaye kupata muafaka wa ghasia zilizokuwa zinashuhudiwa katika nchi hiyo.

Saleh amesema kukabidhi kwake madaraka anaamini kutaleta mapinduzi katika nchi hiyo na kutaka uhuru, usalama na uimara wa nchi hiyo uendelee kwa ajili ya ustawi wa wananchi wote wa Yemen.

Kiongozi huyo ambaye amekaa madarakani kwa miongo zaidi ya mitatu aliingia matatani wakati ambapo wimbi la mageuzi lilipozikumba nchi za Kiarabu na kuchangia uwepo wa mapinduzi katika mataifa hayo.

Saleh amewataka wananchi wa Yemen kuwa bega kwa bega na Uongozi mpya nchini humo ili kuweza kukabiliana na ugaidi kwanza na kisha kuutokomeza Mtandao wa Al Qaeda unaochangia hofu ya usalama.

Rais mpya ambaye atachukua jukumu la kuongoza Yemen kwa miaka miwili ni Hadi kutekeleza maamuzi ambayo yalifikiwa na Viongozi wa Nchi za Ghuba ambazo zilisimamia mazungumzo ya upatanisho kumaliza machafuko.

Rais Hadi baada ya kukabidhiwa rasmi hatamu ya kuongoza nchi hiyo akaweka bayana anahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi ili kuweza kuimarisha uchumi wa taifa hilo unaoonekana kutetereka kwa sasa.

Hadi amesema huu si wakati wa kuendeleza tofauti ambazo wanazo wananchi badala yake watumie fursa hii kurejesha mshikamano walionao na kuhakikisha nchi hiyo inasonga mbele kwa sasa.

Rais Abdrabuh Mansur Hadi alichaguliwa kwenye uchaguzi wa tarehe 21 February akiwa mgombea pekee na kisha kupata asimilia 99.8 ya kura zote huku wananchi waliojitokeza wakiwa ni asilimia 60 pekee.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.