Pata taarifa kuu
YEMEN

Raisi mteule wa Yemen Abdrabuh Mansur Hadi kula kiapo

Raisi mteule wa Yemen Abdrabuh Mansur Hadi ambaye awali alikuwa makamu wa raisi, anatarajia kuapishwa siku ya jumamosi kama raisi mpya wa nchi hiyo kabla ya uzinduzi wa uongozi mpya na kukabidhiwa rasmi madaraka siku ya jumatatu.

Mfuasi wa raisi mteule wa Yemen akiwa amebeba picha ya Abd Rabbu Mansur Hadi
Mfuasi wa raisi mteule wa Yemen akiwa amebeba picha ya Abd Rabbu Mansur Hadi REUTERS/Mohamed al-Sayaghi
Matangazo ya kibiashara

Kiapo hicho kinafuata baada ya Tume huru ya uchaguzi nchini Yemen kumtangaza Mansur Hadi kuongoza kwa kura na kuwa mgombea pekee katika uchaguzi aliyejizolea asilimia 99 ya kura halali.

Raisi mteule Mansur Hadi anatakabidhiwa madaraka na aliyekuwa raisi wa yemen,Abdulah Salleh siku ya jumatatu chini ya mpango wa makubaliano ambapo raisi Salleh aliridhia kujiuzulu kama kinga ya kufunguliwa mashtaka juu ya vifo vya mamia ya raia katika kipindi cha maandamano dhidi ya utawala wake uliodumu kwa miaka 33.

Naibu Waziri wa Habari Abdo Janadi alieleza kuwa Raisi Saleh ambaye kipindi chake cha uongozi kinafikia ukomo anaendelea na matibabu huko nchini marekani kufuatia majeraha aliyopata katika mlipuko mwishoni mwa mwezi june lakini anatarajiwa kujielekeza Yemen kukamilisha makabidhiano hayo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.