Pata taarifa kuu
Syria-Machafuko

Shirika la msalaba mwekundu laingilia kati kuhakikisha machafuko yanasitishwa nchini Syria

Shirika la Msalaba Mwekundu lipo kwenye mazungumzo na serikali ya Syria pamoja na waasi katika kuhakikisha kuwa wanamaliza machafuko yanayoendelea na wao waweze kutoa misaada kwa wanawake na watoto wanaoteseka katika Jiji la Homs.

Mashambulizi ya jiji la Homs
Mashambulizi ya jiji la Homs REUTERS/Handout
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo haya yanaombwa wakati huu ambapo Wanaharakati wakiendelea kutoa takwimu za mauaji ambayo yanatekelezwa na wanajeshi watiifu kwa Rais Bashar Al Assad wanaokabiliana na waandamanaji kwenye Jiji la Homs.

Licha ya juhudi ambazo zinaendelea kuchukuliwa lakini bado zimeonekana kugonga mwamba kwa sasa na hapa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton ameweka bayana uamuzi wa kuweka vikwazo zaidi kwa serikali ya Damascus.
 

Mapema Rais Assad alinukuliwa kwa mara nyingine akituhumu mataifa ya magharibi kwa kufadhili makundi ya kigaidi kifedha na hata kwa silaha.

Hamkani imeendelea kuwa si shwari nchini Syria kwani serikali imeendelea kusistiza inapambana na magaidi huku mataifa ya magharibi yakishinikiza kumaliza kwa umwagaji damu na hata kuondoka madarakani kwa Rais Bashar Al Assad.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.