Pata taarifa kuu
Ugiriki-Umoja wa Ulaya

Umoja wa Ulaya waonekana kuwa tayari kuipa mkopo serikali ya Ugiriki inayo kabiliwa na ghasia za maandamano

Umoja wa nchi za ulaya umeoneka kuwa tayari kutoa mkopo mpya kwa nchi ya Ugiriki baada ya nchi hiyo kupitisha hatua za kubana matumizi kwa lengo la kupata mkopo huo unaohitajika ili kuinusuru nchi kiuchumi

Vionkgozi wa Umoja wa Ulaya na mkuu wa IMF
Vionkgozi wa Umoja wa Ulaya na mkuu wa IMF
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu wa Ugiriki Lucas Papademos anaungana na mawaziri wengine wa uchumi wa jumuiya ya Ulaya wanaokutana huko Brussels Ubelgiji katika mazungumzo ambayo serikali ya Ugiriki inataraji yatatoa ruksa kwa nchi hiyo kupatiwa mkopo wa Euro bilioni 230.

Waziri wa uchumi wa nchi hiyo Evangelos Venizelos amesema kuwa kwa sasa Ugiriki inashuhudia kile kipindi kirefu cha hali mbaya ya kiuchumi iliyokuwa ikishuhudiwa nchini humo kikifikia kikomo hii leo, kipindi ambacho hakikuinufaisha uchumi wa Ugiriki wala ukanda unaotumia sarafu ya Euro.

Kwa upande wake mshirika wa Ufaransa Francoir Baroin amesema kuwa tayari wanakila kitu kinachohitajika kuhusu makubaliano hayo baada ya miezi sita ya mgogoro ambao umeshuhudia wajumbe wa umoja wa Ulaya wakistahimili anguko la Ugiriki na mapendekezo ya kuiokoa kutokana na kuyumba kwa uchumi.

Washirika wa umoja wa Ulaya wanaiona Ugiriki kama muathirika wa kiuchumi kutokana na matumizi mabaya ya fedha yanayofanywa na viongozi wa juu wenye nguvu kisiasa jambo ambalo waziri mkuu wa Italia Mario Monti juma lililopita ameliita kuwa ni orodha kamili ya makosa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.