Pata taarifa kuu
NEW YORK-SYRIA

Baraza la Usalama lapitisha maazimio kulaani mauaji nchini Syria na kutaka kusitishwa kwa machafuko nchini humo

Nchi wanachama 137 za baraza la usalama la Umoja wa mataifa zimekubalina kkwa kauli moja kupitisha maazimio ya kulaani kile kinachoendelea nchini Syria huku nchi kumi na mbili zikiwemo China na Urusi zikipinga maazimio hayo ambayo yamefikiwa na baraza la usalama.

Bashar Jafa’ari balozi wa Syria kwenye Umoja wa mataifa akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo
Bashar Jafa’ari balozi wa Syria kwenye Umoja wa mataifa akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo UN Photo/Eskinder Debebe
Matangazo ya kibiashara

Nchi za China na Urusi zimeendelea kushikilia msimamo wao wa kufanyika kwa mazungumzo katika kumaliza mgogoro wa Syria huku nchini nyingine zikiongozwa na Marekani zikiunga mkono maazimio ya Jumuiya ya Umoja wa nchi za kiarabu yanayomtaka rais Asad kuondoka madarakani na kupisha uchaguzi mkuu.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon ameendela kuyaonya mataifa ambayo yanapinga maazimio yoyote ya baraza la usalama kuhusu hatua za kuchukuliwa dhidi ya serikali ya Syria akisema kuwa kufanya hivyo ni kuruhusu serikali hiyo kufanya inachotaka dhidi ya wananchi wake.

Licha ya kupitishwa kwa maazimio hayo baadhi ya nchi ambazo hazikushiriki kabisa kwenye upigaji kura wa maazimio hayo zimependekeza kutochukuliwa kwa maamuzi ya jazba kuhusu hatua za kuchukua kuhusu Syria na badala yake wametaka mazungumzo yatumike.

Abdullah Hussain Haroonni ni balozi wa Pakistan kwenye Umoja wa mataifa na anataka baraza hilo kutochukua maamuzi ya hasira badala yake mazungumzo yanaweza kumaliza mzozo huu.

Wakati mkutano huo ukiendelea mara kadha Balozi wa Syria kwenye Umoja wa Mataifa Bashar Jaffar aliingilia kati uamuzi huo akisema baraza hilo halina mamlaka ya kupitisha maazimio yoyote kuhusu nchi yake kwakuwa hakukuwa na sheria ambayo iliundwa kutekeleza upitishwaji wa maazimio hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.