Pata taarifa kuu
TUNISIA

Waziri mkuu wa Tunisia ataka nchi zote kuvunja uhusiano wa kibalozi na Syria.

Waziri mkuu wa Tunisia Hamadi Jebali ametoa wito kwa nchi zote kuvunja uhusiano wa kibalozi na nchi ya Syria kwa kuwafukuza mabalozi wa nchi hiyo katika mataifa ya Kiarabu kutokana na machafuko yanayoendelea nchini humo. 

Waziri mkuu wa Tunisia Hamadi Jebal
Waziri mkuu wa Tunisia Hamadi Jebal alarabiya.net
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika mkutano wa majadiliano kuhusu usalama wa nchi za Mashariki ya kati uliofanyika katika mji wa Munich Ujerumani, waziri Jebali amesema kuwa raia wa Syria hawatarajii maelezo marefu wakati huu kutoka kwao badala yake wanataraji vitendo thabiti.

Jebali ameongeza kuwa kura ya turufu iliyopigwa a nchi za Urussi na China siku ya jana dhidi ya azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa UN lenye lengo la kusitisha vurugu umedhihirisha kuwa mfumo wa baraza hilo umevunjwa na hivyo baraza hilo litazame upya mfumo huo wa maamuzi.

China na Urrusi hapo jana zilipiga kura ya turufu dhidi ya azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa UN linalotokana na mpango wa jumuiya ya nchi za kiarabu kumtaka rais Bashar al Assad kukabidhi madaraka kwa makamu wake ili kupisha demokrasia hatua ambayo wanaharakati wa haki za binadamu wamesemakuwa ni kumpa kibali rais Assad kuendelea kufanya mauaji.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.