Pata taarifa kuu
NIGERIA

Msemaji wa kundi la Boko Haram akamatwa na Polisi nchini Nigeria

Kikosi maalumu cha Polisi nchini Nigeria kimetangaza kufanikiwa kumkamata msemaji wa kundi la Boko Haram Abu Qaqa ambaye mara kadhaa ndie amekuwa akitoa taarifa mara baada ya kundi hilo kutekeleza mashambulizi.

Kiongozi wa kundi la Boko Haram, Iman Abubakar Shekau
Kiongozi wa kundi la Boko Haram, Iman Abubakar Shekau REUTERS/IntelCenter/Handout
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taasisi ya usalama wa Taifa nchini Nigeria, imesema kuwa Qaqa alikamatwa kaskazini mwa nchi hiyo katika mji wa Kaduna nyakati za asubuhi wakati akiwa kwenye harakati za kutaka kukimbia mtego wa Polisi.

Hata hivyo taasisi hiyo imeongeza kuwa japokuwa wanamshikilia msemaji huyo wanaendelea kumuhoji ili kuweza kubaini ni nani hasa ambaye wanamshikilia na kama kweli wamemkamata kiongozi sahihi wa kundi hilo.

Abu Qaqa anatajwa kuwa moja kati ya watu muhimu kwa kundi hilo ambaye mara zote amekuwa akitoa taarifa za kundi hilo na mipango ambayo imekuwa ikipangwa naviongozi wake kwa waandishi wa habari.

Kukamatwa kwa mmoja wa viongozi hao kumepokelewa kwa hisia tofaurti nchini humo, huku baadhi ya watu wakihoji hatua ambazo zilipelekea kukamatwa kwa kiongozi huyo na kama ni mtu sahihi kwa sasa kuweza kuisaidia serikali kuwapata wafuasi wengine wakundi la Boko Haram.

Kiongozi huyo anakamatwa wakati ambapo kundi la Boko Haram limekuwa likifanya mashambulizi makubwa kaskazini mwa nchi hiyo kwenye mji wa Kano ambapo katika shambulio la hivi karibuni liliua watu zaidi ya 185.

Serikali inayoongozwa na rais Goodluck Jonathan imekuwa katika shinikizo kubwa toka kwa wanasiasa na jumuiya ya kimataifa wakimtaka kuongeza juhudi zaidi za kuwasaka wapiganaji wa kudni hilo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.