Pata taarifa kuu
SYRIA

Mauaji zaidi yaripotiwa nchini Syria wakati Umoja wa Mataifa ukishindwa kuafikiana kuhusu hatua za kuchukua

Wakati nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakishindwa kuafikiana kuhusu hatua za kuchukua dhidi ya serikali ya Syria, kumeendelea kuripotiwa mauaji zaidi ya raia katika miji mbalimbali nchini humo.

Moja ya maandamano ya wananchi wa Syria kuipinga serikali
Moja ya maandamano ya wananchi wa Syria kuipinga serikali REUTERS/Handout
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la msalaba mwekundu nchini Syria, limesema kuwa zaidi ya watu 68 wameuawa mapaka kufikia jana katika miji ya Homs, Deraa na Idlib ambako majeshi ya serikali yameendelea kuweka doria.

Kwenye ripoti hiyo ya msalaba mwekundu imeeleza kuwa miongoni wa watu waliouawa ni wanajeshi 14 wa jeshi huru la Syria ambalo limeasi serikali ambapo waliuawa katika mji wa wady Barada kusini mwa mji wa Damascus.

Mbali na ripoti za shirika hilo, wanaharakati nchini humo wamesema kuwa zaidi ya watu mia mbili wameuawa mpaka sasa toka siku tatu zilizopita na kuongeza kuwa wanajeshi wa serikali wamekuwa wakipita nyumba hadi nyumba na kuwakamata watu.

Mauaji hayo yanatokea wakati ambapo siku ya Jumanne Baraza la Usalama lilikutana kujadili hatua za kuchukua dhidi ya Syria lakini walishindwa kuafikia kwa kile kilichoelezwa baadhi ya mataifa yenye kura za turufu kupinga kutumika kwa nguvu za kijeshi.

Nchi ya Urusi na China zimeendelea kusisitiza msimamo wao wakutaka kufanywa kwa mazungumzo ili kunusuru nchi hiyo kutumbukia kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Umoja wa nchi za Kiarabu wenyewe umeendelea kulitaka Baraza la Usalama kumlazimisha rais Bashar al-Asad kuondoka madarakani hatua ambayo iliungwa mkono na nchi za Ufaransa, Marekani na Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.