Pata taarifa kuu
MAREKANI-SYRIA

Nchi wanachama wa Baraza la Umoja wa mataifa zashindwa kuafikiana kuhusu hatua za kuchukua dhidi ya Syria

Kwa mara nyingine tena nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamemaliza mjdala wao kuhusu hatua za kuchukua dhidi ya Serikali ya Syria bila kufikia muafaka huku nchi za China na Urusi zikiendelea kushikilia msimamo wao.

Wajumbe wa mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakijadili jambo baada ya kumalizika kwa kikao cha jana
Wajumbe wa mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakijadili jambo baada ya kumalizika kwa kikao cha jana UN Photo/Mark Garten
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo wa hapo jana ulipokea mapendekezo ya Jumuiya ya Umoja wa nchi za Kiarabu ambao umetaka Baraza la Usalama kuukubali mpango ambao umependekeza rais Bashir al-Asad aondoke madarakani kwa hiari na kuitisha uchaguzi mkuu.

Mara baada ya kupokea taarifa ya Umoja wa nchi za Kiarabu, Baraza hilo pia lilipata nafasi ya kupokea mapendekezo ya nchi ya Urusi kuhusu kushughulikia mgogoro wa nchi ya Syria na baadae wanachama kuanza kujadili mapendekezo yote mawili bila ya kufikia muafaka.

Wajumbe walikataa baadhi ya mapendekezo ya Umoja wa nchi za kiarabu ikiwemo swala la kupendekeza kutumia nguvu za kijeshi kuivamia nchi hiyo jambo ambalo nchi ya Urusi na China zimepinga vikali.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema kuwa hadhani kama mapendekezo ya nchi yake yanataka kubadilishwa kwa utawala wa Syria hapana bali tunataka kuona mauaji dhidi ya raia wasio na hatia yanasitishwa.

Kwa upande wa nchi ya China yenyewe moja kwa moja imeungana na nchi ya Urusi na kukataa matumizi ya nguvu za kijeshi wala kubadilishwa kwa utawala kwa kile ilichodai kuwa kufanya hivyo ni kukiuka mkataba wa kimataifa ambao uliazimiwa na Umoja huo kuhusu kuheshimu mamlaka ya nchi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.