Pata taarifa kuu
MAREKANI-SYRIA

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN, kuijadili Syria

Watu zaidi ya mia moja wameripotiwa kuuawa nchini Syria siku ya Jumatatu katika machafuko yanayoendelea kati ya waandamanaji wanaoipinga Serikali na majeshi ya nchi hiyo.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akizungumza wakati wa mkutano wa Bazara la Usalama
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akizungumza wakati wa mkutano wa Bazara la Usalama UN Photo/Ryan Brown
Matangazo ya kibiashara

Hapo jana usiku kumeripotiwa kuzuka mapigano katika miji kadhaa ya nchi hiyo ikiwemo Deraa, Homs na kusini mwa mji mkuu Damascus ambapo wanajeshi walioasi walijaribu kuiweka kwenye himaya yao miji hiyo.

Wakati mapigano hayo yakiendelea, nchi ya Marekani yenyewe imeendelea kusisitiza kutoitambua Serikali ya Syria kama Serikali halali kwa kile ilichodai ni kuendelea kutokea kwa machafuko na kuuawa kwa wananchi wasio na hatia na vikosi vya nchi hiyo.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jim Carney, amesema kuwa nchi yake inaamini kuwa rais Asad na utawala wake siku zao zinahesabika na kwamba muda wa wao kuendelea kusalia madarakani unafikia kikomo hivi karibuni.

Hii leo viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa nchi za Kiarabu watakuwa mjini New York Marekani kuwasilisha mapendekezo yao kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hatua ambazo wao wanapendekeza kuchukuliwa dhidi ya utawala wa rais Bashar al-Asad.

Mkutano huo wa Baraza la Usalama unatarajiwa kupkea mapendekezo ya nchi ya Urusi kuhusu hatua za kuchukuliwa dhidi ya Syria na baadae kujadili mapendekezo hayo kabla ya kuyakubali au kuyakataa mapendekezo hayo.

Hata hivyo mpango huo wa Urusi huenda ukapingwa na wajumbe wengine ingawa nchi hiyo inaungwa mkono na taifa la China ambalo nalo linapinga kutumika kwa nguvu za kijeshi dhidi ya utawala huo.

Kwa upande wake Serikali ya Syria imesema kuwa inashangazwa na mataifa ya ulaya kuuona utawala wao kama sumu wakati wao ndio wanaochangia kwa kiasi kikubwa kuendelea kutokea kwa machafuko nchini humo.

Waziri wa mambo ya nje wa Syria amezishutumu vikali nchi wa Umoja wa nchi za Kiarabu kwa kukimbilia kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakati nchi hiyo ilikuwa tayari kumaliza mzozo huo na Umoja huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.