Pata taarifa kuu
SYRIA-DAMASCUS

Vikosi vya Syria vyafanikiwa kurejesha amani mashariki mwa mji mkuu Damascus

Hatimaye vikosi vya serikali ya Syria Vimefanikiwa kurejesha amani katika mji wa Al-Ghouta ulioko mashariki mwa mji mkuu Damascus baada ya kutokea makabiliano makali ya siku mbili mfululizo kati ya vikosi vya serikali na wanajeshi walioasi.

Wanajeshi wa Syria wakiwa katika doria masahriki mwa mji mkuu Damascus
Wanajeshi wa Syria wakiwa katika doria masahriki mwa mji mkuu Damascus Reuters
Matangazo ya kibiashara

Taarifa toka mjini Damascus zinasema kuwa wanajeshi walioasi waliamua kuondoka wenyewe kwenye mji huo baada ya kukabiliana kwa siku mbili na vikosi vya serikali na kuahidi kurejea tena kwenye mji huo kujaribu kuuweka kwenye himaya yao.

Maelfu ya wananchi walionekana kuukimbia mji huo kuhofia kuuawa katika mapigano hayo, ambapo wanaharakati wanaoipinga serikali wamesema kuwa baada ya wanajeshi kuingia kwenye mji huo wamekuwa wakiwaua raia wasio na hatia.

Hata hivyo serikali imekanusha vikali wanajeshi wake kuua raia, badala yake wamewatupia lawama wapiganaji hao kwa kusababisha wananchi kukimbia nyumba zao wakihofia kufa pamoja na kusababisha hali ya hatari kwa saa kadhaa.

Mapigano hayo yanaendelea wakati ambapo baraza la Usalama la Umoja wa mataifa linaendelea kuvutana kuhusu hatua za kuchukua dhidi ya serikali ya rais Asad ambapo baadhi ya nchi zimetaka hatua za kijeshi kuchukuliwa huku nchi ya Urusi na China zikipinga.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameendelea kutoa wito kwa serikali ya Syria kuacha mauaji dhidi ya raia na kuliomba Baraza la Usalama kukubalina kwa kauli moja kuhusu hali ya mambo nchini humo.

Wiki hii viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa nchi za Kiarabu wanatarajiwa kuwasilisha mpango wao kwenye Umoja huo kwa lengo la kuzishawishi nchi zaidi kuwaunga mkono kuhusu hatua za kuchukua dhidi ya Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.